Mwalimu Massawe alikimbia Songea!!!

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2008
Posts
4,768
Reaction score
2,361
Mwalimu Praygod Massawe alipangiwa kazi mjini Songea, Shule iliyopo karibu pal pal Bomba mbili, jirani na kwa Mfaranyaki.
Sehemu hiyo maarufu sana Songea.
Kufika tu akapokelewa na Mwalimu Ngonyani.
Massawe akashangaa, akuliza "aisee unitwa nyani?"
"Hapana" akajibiwa Ngonyani
Punde akatambulishwa kwa Mwalimu Katembo
Massawe akauliza tena"aisee nawee ni tembo"
Akaambiwa " hapana KATEMBO"
Punde tu wakaingia walimu wawili walitambulishwa harakaharaka, Mwalimu Mapunda na Mwalimu Nyoka.
"Sasa aisee na wewe unaitwa nani ndugu yangu" akashangaa Mwalimu Massawe kwa mwalimu mwingine wa jirani
"Aaah mimi ni Mwalimu Mbawala" akajibu mwalimu huyo, Massawe akaendelea kushangaa.
Mwenyeji wake akamshauri kumsubiri Mwalimu Mkuu ampangie mahali pa kulala.
"Usinitanie aisee,Mwalimu Mkuu anaitwa nani mwalimu mwensangu"akauliza Mwalimu Massawe
"Ulipokuja hukuambiwa? akahoji mwenyeji wake
"Huyo anaitwa Mwalimu Mamba"
Masikini Mwalimu Massawe hapo akaona , now zis is too much, hawa jamaa wananipeleka mbugani nini, akaelekea kituo cha basi kurudi Moshi.
 
na kweli huko ni mbugani, majina yote ya wanyama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…