Mwalimu mkuu atunukiwa kinyago cha kutisha baada ya shule yake kushika mkia NECTA

Mwalimu mkuu atunukiwa kinyago cha kutisha baada ya shule yake kushika mkia NECTA

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,093
Reaction score
7,229
attachment.php

Mwalimu mkuu shule ya msingi kamanga Bw.Lucas Nicolaus(Pichani) iliyoko wilaya ya chato amekabidhiwa zawadi ya kinyago cha kutisha (kina sura ya mtu zoba /mburura) baada ya shule yake kuburuza mkia katika matokeo ya mtihani wa taifa (NECTA) wa darasa la saba 2013. Wilaya ya chato huwa na utaratibu wa kuwatunuku zawadi za ngao fedha taslimu kwa shule zilizofanya vizuri na kinyago cha kuogofya kwa shule zilizofanya vibaya. Zawadi hizo ziliztolewa na afisa elimu wa wilaya ya chato Bw.Angasirin Obed Kweka mbele ya baraza la Madiwani wilaya ya chato hapo jana

Mimi nimependa sana utaratibu huu wa kuwatunuku, rai yangu ni kuomba na halmashauri zingine nchini ziige utaratibu huu katika mitihani yote kuanzia shule ya msingi mpaka kidato cha sita,pia na NECTA waige mfano za mtindo huu. wadau manionaje huu mtindo kwani elimu hata ya zile shule kongwe nchini imekuwa ikizidi kushuka siku hadi siku. hii inaweza kuwa njia ya kurudisha hadhi ya elimu yetu kwa kiasi falani.

N.B: Hakuna kuruHUsu kutuma mwakilishi kwenye kupokea zawadi.. mlengwa anatakiwa awe mkuu (kama chato walivyofanya) , makamu au mtaaluma wa shule husika. hii itasaidia kuweka mkazo kwa wasimamizi wa elimu kuwa makini na kazi yao kwa kiasi flani.
Chanzo: Chimbwara
 
Attachments

  • unnamed (24).jpg
    unnamed (24).jpg
    38.2 KB · Views: 8,717
  • unnamed (22).jpg
    unnamed (22).jpg
    37.3 KB · Views: 648
  • unnamed (23).jpg
    unnamed (23).jpg
    38.5 KB · Views: 586
ni hatua nzuri nimeipenda sana,
kinyago hichi kitundikwe eneo la wazi hapo shuleni ili kiwachukize wanafunzi wote wapate motisha wakujitahidi next time tusiwaongeze kinyago kingine chenye sura mbaya zaidi.
 
ahahaa... tena kikiwekwa kwenye meza y mkuu au mtaaluma itakuwa pouwa zaidi, na kingine kwenye eneo la mkusanyiko "assembly ground/smart area " pembeni ya bendera ya Taifa itakuwa vema zaidi.
 
Hahahaha mimi ningetuma mwakilishi kwenda kuchukua hicho kinyago,hakiya nani sitii mguu huko
 
ahahaa... tena kikiwekwa kwenye meza y mkuu au mtaaluma itakuwa pouwa zaidi, na kingine kwenye eneo la mkusanyiko "assembly ground/smart area " pembeni ya bendera ya Taifa itakuwa vema zaidi.

na itungwe nyimbo ya majuto ya kukiimbia kinyago hichi mpaka ufaulu uongezeke ndo tutoe kinyago hicho na tusitishe nyimbo hiyo ya majonzi hapo assemble.
 
Hahahahahah junior.Cux embu pitia apa twende mjini
Umeona enhee... ya ukifika ofisini kwake kama umeingia kwenye chumba cha kutunzia kadava "cadaver room" kama zile za IMTU...ahahaa
 
Last edited by a moderator:
ni hatua nzuri nimeipenda sana,
kinyago hichi kitundikwe eneo la wazi hapo shuleni ili kiwachukize wanafunzi wote wapate motisha wakujitahidi next time tusiwaongeze kinyago kingine chenye sura mbaya zaidi.

Na akirudi shuleni arudishe feedback kwa kuwaonyesha wanafunzi wote zawadi aliyoipokea na ikiwezekana inakuwa inakaa kwa zamu kama ilivyo zamu kwa kila darasa yaani ikifika tu asubuhi kiongozi wa darasa anaenda kuchukua kwa mwalimu wa darasa na kuweka darasani au kwenye mhula wa kwanza darasa ambalo litapata wastani wa chini kuliko madarasa mengine ndio itakuwa mzigo wake huo (ila kasoro kwa darasa la kwanza, pili na tatu ambao bado wadogo wanahitaji motisha ya kutiwa moyo zaidi)
 
Chakushangaza wote wana nyuso za furaha badala ya kusikitika

Hata ukisikitika haisaidii kikubwa inabidi ufurahi maana hilo nalo ni neno ati, unachotakiwa ukitoka hapo ni kwenda kupambana asikipokee tena hicho kinyago
 
Hahahaha mimi ningetuma mwakilishi kwenda kuchukua hicho kinyago,hakiya nani sitii mguu huko

"Terms & conditions to be applied" vigezo na masharti kuzingatiwa,
tumesema hakuna kutuma mwakilishi . kwani miongoni mwa wale viongozi wa ngazi za juu "top layer leaders" kama mkuu, makamu, mtaaluma au nidhamu.
 
Mawaziri watakaoshindwa wajibu wao wanapewa nini. Lazima tujue sababu za kufeli. Waalimu wachache, motisha, vitendea kazi
 
Chakushangaza wote wana nyuso za furaha badala ya kusikitika

Bora utabasamu tu kwenye kupokea ili kupunguza munkari wa mgeni rasmi , kwani kinyume chake unaweza kula za chembe kidevu kwenye hotuba yake mpaka uka poteza kumbukumbu ya jina la shule yake.
 
Mawaziri watakaoshindwa wajibu wao wanapewa nini. Lazima tujue sababu za kufeli. Waalimu wachache, motisha, vitendea kazi

Kwahiyo unatka kusema kuwa na wao wana deserve the same kind of prize kama walimu wa chato...???
 
Back
Top Bottom