A
Anonymous
Guest
Naripoti kutoka Shule ya msingi Upendo Mbezi Louis, kuwa uongozi wa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo pamoja na msaidizi wake namba 2 ni wa ki maslahi binafsi na usio wa ushirikishwaji kwa Walimu wengine, matusi, dharau na kashfa mbalimbali
1. Upangaji wa Walimu kwenye vipindi ni wa ovyo na usio na uwiano, Walimu wengi amewapanga madarasa ya chini ili madarasa ya juu abaki yeye na walimu baadhi kwa ajili ya kupiga pesa za tution japo kuwa kuna Walimu pia hufundisha hizo tution lakini hawapati chochote, darasa la kwanza lina walimu 8, darasa la memkwa lenye wanafunzi 12 lina walimu 4 na darasa la pili lina walimu 10, wakati huo darasa la sita lina walimu 5, la saba lina walimu 3, halafu kweli Mwalimu afundishe vipindi vyote kwa wanafunzi na tutegemee kuna kufaulu hapo?
2. Matumizi ya capitation ( 1,600,000) hayako wazi kwa Walimu wa ngazi za chini hivyo Walimu hawajui chochote juu ya matumizi ya pesa hizo ili hali hawanunuliwi kalamu wala daftari za nukuu hivyo hulazimika kununua kw pesa zao wenyewe, hii sio haki kabisa ukilinganisha n mishahara wanayolipwa.
3. Walimu hawanunuliwi hata chai shuleni alihali pesa za ushuru hukusanywa kila siku
4. Mitihani ya muhula haitungwi na Walimu bali anapeleka mitihani yake ambayo wWalimu wanasema iko chini ya viwango na muda mwingne inakuwa nje na topic ambazo wao wamefundisha. Mitihani hiyo pia hulipiwa na wanafunzi Tsh 1,500 kwa kila mwanafunzi lakini Walimu huwapa sh 5,000 tu kwa ajili ya usahihishaji na alihali mitihani hawajatunga wao.
5. Kwa Maslahi yake ameruhusu baadhi ya walimu kuuza vitu darasani kisha walimu hao humpa pesa, hii inachangia kuzorotesha ufanisi katika ufundishaji.
OMBI LA WALIMU
1. Walimu wanaomba uongozi wa shule ubadilishwe ili kusaidia kuinua taaluma ya shule na kuzuia rushwa na maslahi binafsi
2. Walimu wanamuomba afisa Elimu na Mkurugenzi kufanya uchunguzi juu ya hayo malalamiko na wakigundua kuwa kuna ukweli au uongo basi tafadhali wachukue hatua stahiki.
3. Walimu wanaomba uwiano kwenye kupangiwa vipindi kwani kuna baadhi ya Walimu hufanya kazi kubwa kuliko wengine.
4. Kuna walimu wa kujitolea shuleni wakati kwa ujumla walimu wa kuajiriwa wako 56, hao wa kujitolea ni wa kazi gani?
Naweka kalamu chini nawasilisha hoja kwa mamlaka husika
Ni mimi Kibaraka wa Mtaa.