Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) kimewataka wananchi wa Mkoa wa Morogoro kujiandaa kunufaika na neema ya sera ya viwanda, kikiahidi kurejesha hadhi ya mkoa huo kuwa kitovu cha viwanda kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu Julius Nyerere.
“Morogoro ni mkoa wa kimkakati kwa ajili ya viwanda kwa sababu uko katikati ya Bandari ya Dar es Salaam na Tanga, jambo linalorahisisha usafirishaji wa bidhaa,” amesema Mwalimu.
Ameeleza kuwa viwanda vilivyowahi kujengwa mkoani humo vilikufa, lakini Chaumma imelenga kufufua taswira ya Morogoro kuwa mkoa wa viwanda.