Mwalimu Nyerere alinyimwa VISA na taifa kubwa akaiasa Afrika kufanya mabadiliko

Mwalimu Nyerere alinyimwa VISA na taifa kubwa akaiasa Afrika kufanya mabadiliko

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Tunapoelekea katika mwezi wa kumbukizi ya Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni vyema kutafakari kila neno alilowahi kulitoa.

Katika moja ya hotuba zake kwa wanahabari aliwahi kugusia madhila aliyowahi kupata kama kiongozi wa nchi kwa kunyimwa visa na TAIFA KUBWA.

Hakika inatia simanzi ila ni bullying iliyowahi kuwepo na pengine itakuwepo kwa muda mrefu ujao. Japo alituasa kama waafrika kuleta mabadiliko.

Hayo mambo kabla ya uhuru hayaakisi ukweli uliopo duniani sasa hivi
Hata hivyo Mwalimu alialikwa na kukutana na Rais John Fitzgerald Kenedy Marekani na baada ya Ziara hiyo tuakaona maelfu ya Wamarekani wakija kama Peace Corps kufanya kazi za kujitolea.
 
..Tz tuliwahi kufukuziana maofisa ubalozi na Marekani miaka ya 60.

..Pia tuliwahi kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na Ujerumani Magharibi.

..Vilevile tulikuwa na ugomvi mkubwa na Uingereza kuhusiano na suala la uhuru wa Zimbabwe / Rhodesia. Sina uhakika kama tulivunja mahusiano ya kidiplomasia.

..Tz pia ilivunja uhusiano wa kibalozi na Israel kupinga taifa hilo kukalia kwa mabavu ardhi ya nchi za Kiarabu mwaka 1967.

..Zaidi ya matukio hayo sina taarifa za Tz kuwa na mgogoro mkubwa wa kidiplomasia na mataifa mengine.
 
..Wakati wa kudai UHURU Wakoloni wa Kiingereza walimchongea ili Wamarekani wamnyime visa.

..Wamarekani wakampa Mwalimu Nyerere visa yenye masharti iliyomuwezesha kwenda UN kudai uhuru wa TANGANYIKA.
Mleta hoja kaambiwa aoneshe ushahidi amedai tuendelee kuperuzi tu.Tutaona humohumo.
 
Tunapoelekea katika mwezi wa kumbukizi ya Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni vyema kutafakari kila neno alilowahi kulitoa.

Katika moja ya hotuba zake kwa wanahabari aliwahi kugusia madhila aliyowahi kupata kama kiongozi wa nchi kwa kunyimwa visa na TAIFA KUBWA.

Hakika inatia simanzi ila ni bullying iliyowahi kuwepo na pengine itakuwepo kwa muda mrefu ujao. Japo alituasa kama waafrika kuleta mabadiliko.

Kupewa visa ya masharti ni tofauti na kunyimwa visa. Tofautisha ndugu yangu. Visa zote za kila nchi zina masharti yake. hata za kwetu Tanzania zina masharto yake.
Mwisho kasema, " kama kuna haja ya mabadiriko, leteni mabadiriko..."sasa shida iko wapi ? leteni, fanyeni mabadiriko.
 
Unataka kuipamba?Kumpa kiongozi wa nchi visa yenye masharti unaona ni jambo dogo?
 
Unataka kuipamba?Kumpa kiongozi wa nchi visa yenye masharti unaona ni jambo dogo?
Haya ni mambo ya kawaida, hata sasa hawa waingereza wanayo kitu inaitwa VIP Delegate visa na masharti yake ni kwamba Raisi wa nchi yeyote anayewatembelea hawezi kusafiri na lundo la wasaidizi zaidi ya 20 na visa haitazidi zaidi ya siku tatu baada ya kufika huko.. hebu soma hapa nisikuchoshe ndugu yangu: VIP Delegate Visa.
 
Back
Top Bottom