Mwalimu Nyerere: Hii Katiba ya Tanzania, tukimpata Rais asiye na busara anageuka kuwa Mungu

Mwalimu Nyerere: Hii Katiba ya Tanzania, tukimpata Rais asiye na busara anageuka kuwa Mungu

lendila

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
5,806
Reaction score
4,370
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?

"Katiba hii imenipa Madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu". - Mwl. Nyerere 1982.
 
Katiba ya USA iliandikwa mwaka 1787 na inatumika mpaka leo. Mwl Nyerere na uwanafalsafa wake wote alichokishindwa ni kutuachia katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi kwa miaka mingi. Ila kutuambia eti akija mtu mwenye nia tofauti katiba haifai ni udhaifu mkubwa. But kila kitu alichofanya nyerere kinaonekani ni chakishujaa
 
Ndio maana katiba siyo agenda tena pamoja na kuea imegharimu mabilion ya walipa kodi.
 
Katiba ya USA iliandikwa mwaka 1787 na inatumika mpaka leo. Mwl Nyerere na uwanafalsafa wake wote alichokishindwa ni kutuachia katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi kwa miaka mingi. Ila kutuambia eti akija mtu mwenye nia tofauti katiba haifai ni udhaifu mkubwa. But kila kitu alichofanya nyerere kinaonekani ni chakishujaa

Udhaifu wake umekwisha ubaini,wewe binafsi umechukua hatua gani?
 
Mwalimu nyerere aliwai kusema kuwa hii katiba yetu,inampa mno madaraka makubwa sana,mwalimu alisema kuwa kama tukimpata rais asiyekuwa na busara,kwa katiba hii rais anajeuka kuwa mungu,unakubaliana na kauli ya mwalimu nyerere?
Hiyo haina ubishi tena....mbona dalili zipo wazi kwa sasa?
 
Mwalimu nyerere aliwai kusema kuwa hii katiba yetu,inampa mno madaraka makubwa sana,mwalimu alisema kuwa kama tukimpata rais asiyekuwa na busara,kwa katiba hii rais anajeuka kuwa mungu,unakubaliana na kauli ya mwalimu nyerere?
Kama yy aliona katiba inampa rais kua mungu mtu na yy ndie aliekua raise mbona akubadili katiba ili kumuondolea kazi kubwa rais? Asitueke Watanzania kama wapofu wa macho. Yeye ndio aliusika na katiba mbovu tulio nayo.
 
Back
Top Bottom