Ni bora kuwa na macho ukaona kuliko kusimuliwa uzuri wa kitu maana wapambe ni nuksi wanakusifu hata ukitoka uchi watakuambia umependeza maana huna macho
Viongozi wengi kwa sasa hawapitii sieve/chekeche la ubora wao bali kwa kujuana tu unaweza kuwa mtu wa ngazi yeyote ndani ya nchi hii hata za nafasi za kuteuliwa na raisi hata uwe huna elimu yoyote unawza ukawa mkuu wa wilaya, mkoa, meneja, mwenyekiti wa bodi, mkuu wa shule, mkuu wa chuo, mkuu wa idara katika halmshauri zetu, mkuu wa kitengo nyeti cha wasomi, mkuu wa kitu chochote au hata wanaweza kuamua kukuanzishia tasisi ili uwe mkuu na wewe upate kula na kunyonya wananchi.
Haya yote yataisha tu tuombe uzima kwa watakao kuwa hai watasema maana nchi hii imeoza kila idara na kila mahali ni kujuana tu na kama unabisha subiri maana tabia hii inakuwa kwa kasi ya ajabu katika nchi yetu na kama huna mtu kitu kidogo utoe ndo jina litawekwa katika white list lasivyo utakuwa katika black list katika maisha yako yote bila kujali elimu yako, ujuzi wako wala umuhimu wako katika maendeleo ya taifa hili.