Mwalimu wa Historia alituongopea?

Mwalimu wa Historia alituongopea?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Miaka mingi imeshapita lakini ningali nikikumbuka bara bara!

Tulipokuwa "High School", kwenye moja ya somo la Historia, Mwalimu wetu alituambia kuwa waliokijenga Chuo Kikuu cha Makerere ni Wamarekani.

Miaka hiyo, Marekani ilianza utaratibu wa kuwapeleka Marekani baadhi ya Waafrika kutoka Afrika Mashariki kwa ajili ya Elimu ya Juu. Hilo lilipelekea Uingereza kuijia juu Marekani, kwamba kwa kuwapeleka Waafrika Marekani, kutafanya kuwa vigumu kuendelea kuwatawala.

Sababu ni kuwa watakapokuwa Marekani, wataweza kuchangamana na Wazungu na hivyo kuanza kuwaza kama wao, na wakiwa na fikra kama zao, hawatakubali tena kuendelea kutawaliwa. Kwa hiyo, Uingereza ikaiambia Marekani kuwa badala ya kuwapeleka Waafrika Uzunguni, wawajengee Chuo chao huko huko kwao, ndiyo Chuo Kikuu cha Makerere kikajengwa.

Hayo yana ukweli au Mwalimu alitulisha matango pori?

Nimetafuta mtandaoni lakini sijaona ushawishi wo wote wa Marekani juu ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Makerere?

Mwalimu wetu wa "High School" somo la Historia alitudanganya?
 
Kilijengwa na nan???
 
Back
Top Bottom