Mwalimu wa IT, Physics na Mathematics natafuta kazi

joumer

Member
Joined
May 2, 2014
Posts
45
Reaction score
6
Habari wapendwa.

Mimi ni Mtanzania ambaye nimebahatika kumaliza elimu ya Sayansi ya Kompyuta (BS CS) katika chuo kikuu kimoja hapa Tanzania.

Mimi siyo mwalimu kwa taaluma (professional) ila nimekuwa katika tasnia ya elimu kwa zaidi ya miaka mitano nikifundisha masomo ya Physics na Mathematics. Pia nimekuwa mwalimu wa Vyuo vya Ualimu kwa takribani miaka mitatu sasa nikifundisha masomo ya MATHEMATICS, PHYSICS, ICT na EMT kwa ngazi ya DIPLOMA na TEHAMA na HISABATI kwa ngazi ya CHETI.

Nimejaribu kutafuta nafasi serikalini ila nimegonga mwamba kwani sina vyeti vya ualimu. Wanajamii wenzangu naomba kama kuna chuo/shule chochote kina nafasi ya kazi na kinatafuta mwalimu naomba mnijulishe. Pia nina uwezo wa kufundisha masomo ya progamming language mbalimbali. Natanguliza shukrani za dhati.

Ahsanteni!
 
Mkuu, jiunge angalau na Post Graduate Diploma ya Open University ili uweze kushindana katika soko la ajira ya ualimu... mie ni Graduate Bsc. Ed. (Physics&Maths) lakini ajira imekuwa ngumu...
 
Nakushauri ujaribu Shule za St maries kidogo zina wapa watu nafac hasa kwa masomo yako hayo bila kuangalia taaluma ya Ualimu.. best regards
 
Mkuu, jiunge angalau na Post Graduate Diploma ya Open University ili uweze kushindana katika soko la ajira ya ualimu... mie ni Graduate Bsc. Ed. (Physics&Maths) lakini ajira imekuwa ngumu...

Ahsante kwa ushauri
 
jitahd kk...ualimu ni professional.. tafuta open university..
 
Nimemaliza elimu ya sayansi?? ndo nini hiki,chuo kikuu gani hiki ambacho hujui hata level yako ya elmu
 
Mkuu, jiunge angalau na Post Graduate Diploma ya Open University ili uweze kushindana katika soko la ajira ya ualimu... mie ni Graduate Bsc. Ed. (Physics&Maths) lakini ajira imekuwa ngumu...
Na huu ndio wakati wa kuomba, fanya hivyo.
 
Mkuu, jiunge angalau na Post Graduate Diploma ya Open University ili uweze kushindana katika soko la ajira ya ualimu... mie ni Graduate Bsc. Ed. (Physics&Maths) lakini ajira imekuwa ngumu...

are you serious Bsc.Ed phy&maths hujapata ajira? ulimaliza mwaja gani? ulifaulu kweli.

kama ulifaulu vizuri andika barua faster kwa mkono uombe ajira utaajiriwa faster kuna uhaba sana physics
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…