Muhitimu wa kidato cha sita aliyeshindwa kujiunga na chuo cha ualimu kwa kukosa ada, Bernard Mwakajila ametengeneza ‘A’ 1OO za somo la hisabati katika shule ya Sekondari Kimara iliyopo Wilayni Ubungo mkoani Dar es Salaam.
Mhitimu huyo, anasema aliingia katika shule hiyo kwa lengo la kusaidia wanafunzi wengi kufaulu somo hilo, ikiwa ni sehemu ya ndoto zake tangu akiwa shuleni.
Soma pia:
Serikali imekamilisha ujenzi wa shule ya sekondari, Wanafunzi wamezeshwa script iliyowasaliti kumsifia Rais Samia
View attachment 3456549
Akizungumza na mwandishi wa makala hii katika mahojiano maalum huko shuleni kwao juzi, Mwakajila ambye pia ni maarufu kwa jina la “Mgalatia wa Hesabu” anasema yeye ni miongoni mwa waliologwa na somo hilo.
Katika simulizi yake anasema kati ya wanafunzi wake 457 waliofanya mtihani wa taifa kidato cha pili mwaka jana kati yao 100 walifaulu somo la hisabati.
Anaposimulia namna alivyofanikisha kufaulisha wanafunzi wengi katika somo hilo, mwalimu huyo anaamini jambo la kwanza ni kumtanguliza Mungu mbele pamoja na ushirikiano mzuri kati yake, wanafunzi na uongozi wa shule.
“Ninapofana kazi katika mazingira mazuri ninakuwa sawa kabisa kufundisha hisabati, kwahiyo kutokana na mazingira mazuri yaliyopo katika shule hii, wote tukajikuta tunaimba wimbo mmoja lazima tufanye vizuri kwenye hesabu” anasema Mwakajila huku anasisitiza hilo pia limetokana na juhudi za pamoja.