Mwalimu wa sekondari aburuzwa mahakamani kwa kumchinja mtoto wake kwa panga

Mwalimu wa sekondari aburuzwa mahakamani kwa kumchinja mtoto wake kwa panga

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Mwalimu mmoja wa sekondari nchini Kenya Stephen Wachira Wangara mwenye umri wa miaka 43, amefikishwa mahakamani kwa kosa la kumuua mtoto wake wa miezi 7 kwa kumchinja kwa panga.

Wakielezea mbele ya mahakama mashahidi watano wa tukio hilo wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya usalama Kaunti ya Kirinyaga, Maina Muriuki walimweleza Jaji Lucy Gitari wa Mahakama Kuu ya Kerugoya, jinsi mtuhumiwa huyo alivyoua mtoto wake,

Bwana Maina aliieleza mahakama kuwa mwili wa mtoto huyo ulikuwa umeeekwa ndani ya gunia ukiwa na damu, nje ya nyumba ya Bw Wangara, na kando ya mwili huo kuliwa na panga ambayo ilitumiwa kumuua mtoto huyo.

Shahidi mwingine Joseph Muriithi alisema wakati wa tukio hilo alikuwa shambani kwa Bw. Wangara akifanya kibarua, na mtuhumiwa huyo kwenda akiwa na madoa ya damu, na muda mfupi baadaye alisikia kelele kutoka kwenye nyumba ya mwalimu huyo.

Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Machi 1, 2018, ambapo itasikilizwa tena.

Bw Wangara ambaye ni mtuhumiwa ni baba wa watoto wawili na mwalimu katika shule ya upili (sekondari) ya Gituya

Chanzo: EATV
 
Sasa kama huko Kenya walimu wanachinja watoto wao je hawa waliopo Tanzania na tumewapa majukumu ya watoto wetu tunauhakika wa kuwatendea vema. Wenye shule kuweni makini hawa watu ni makatili sana. Nafasi au vyeo vya uangalizi watoto zibaki kwa WaTanzania tu kama inavyokuwa nchi nyingine wao wabaki kufundisha tu na wawe na vibali vya kufanya kazi nchini kwani wengi hawana na polisi wakifika kukagua hujificha.
 
Back
Top Bottom