Mwalimu wa Shule ya Msingi aliepata Div IV ya Pts 28 kidato cha nne anaandaa msomi gani hapo baadae?

Huu Uzi ni mzuri ila umeunyima nyama za kutosha. Ungefunguka zaidi kidogo mkuu maana naona watu upande wa pili leo hakuna mijadala mizito ila huu upo sawa!
Tatizo hapa ni kuandaa janga na tutalila sisi na ndugu zetu. Tunaandaa wapiga kura basi. Wanasayansi, wanasheria, madaktari na wataalam wengine kuna siku tutaimport toka kenya, uganda na malawi!
 
Bila shaka mtoa mada si mtanzania na pia hajawahi kusumbua akili yake kutafuta ukweli wa kile anachokihoji. Tangu uhuru hadi sasa walimu wa shule ya msingi ni wale waliohitimu darasa la VII na form IV wenye div IV au III na ninaamini hata yeye kafundishwa na hao. Anachotakiwa kufanya mtoa mada ni kujadili namna ya kuboresha elimu nchini na siyo kudharau wale waliomfikisha hapo alipofikia. Licha ya hayo umeshasoma falsafa ya Plato wewe? Plato aligawa watu kulingana na IQ zao na hata kazi zao zinategemea na hizo IQ, kama unalijua hilo unafikiri walimu wanaingia ktk group lipi kati ya hayo? Kwa ujumla ninaamini kuwa wataalamu wote tulionao leo TZ ni zao la walimu hao tunoawadharau leo. kuna mwalimu wangu pale RUCO Prof Komba ambaye sasa ni mkuu wa chuo cha SAUT-Songea aliwahi kutueleza kuwa ktk maisha yake ya elimu hakuna mwalimu anamheshimu na kumthamini kama yule aliyemfundisha shule ya msingi hususa darasa la I & II,hawa ni walimu haohao unaowadharau wewe. Huyo Prof Komba kafundishwa na hao na leo hii ni Prof.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…