Mwalimu wa Simba, Pablo ameonyesha uwezo wake mkubwa aliokuwa akiutumia Real Madrid

Chilojnr

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
308
Reaction score
1,352
1. Mwalimu wa Simba, Pablo ameonyesha uwezo wake mkubwa aliokuwa akiutumia Real Madrid kwa kuanza na formation ya 4 4 2 ila baada ya kuona Yanga wamekaa sana nyuma, akabadilika na kuanza kutumia 4 3 3. Yaani kwa kifupi alitoka kwenye ule mfumo wa Simba ya nchi kavu na kuhamia Simba ya baharini aliyopewa Red Arrows.

2. Yanga walianza vizuri kwa kutumia mfumo wa 4 5 1 ila baada ya kuona viungo vya vimekufa, sasa wakaanza kutumia mfumo wa 6 3 1 kwa sababu Simba walionekana kuwa bora sana kwenye kupeleka mashambuli.

3. Bernard Morisson...WHAT A MATCH...matokeo mazuri ya Simba yalipitia kwa huyu jamaa, licha ya kufunga mabao mawili lakini alionyesha yeye ni mtu wa aina gani. Aliifanya mechi ajuavyo yeye kiasi cha mabeki wa Yanga kutokujua ni lipi lilitakiwa kufanywa.

4. Leo Feisal Toto hakuonekana kabisa. Nadhani ni kwa sababu timu iliamua kubaki nyuma badala ya kwenda mbele. Kuna kipindi sikuona umuhimu wake kwenye mechi kwa kuwa iliweza kupita hata dakika 20 hakuwa amegusa mpira.

5. Golikipa Diara ni wa aina yake. Niseme tu kwa sasa mbali na Manula huyu ndiye kipa anayeongoza kwa ubora. Leo ameokoa michomo mingi sana, bila yeye, nadhani ile kipigo cha Bayern dhidi ya Barcelona mwaka jana tungeweza kukishuhudia taifa.

6. BRAVO BANGALA...Nadhani huyu ndiye Man of the match kwa upande wa Yanga, alijitahidi sana kukata mawasiliano pale katikati mpaka Simba ilipoamua kutumia upande wa Bernard Morosson ambao ulileta matokeo ya mabao matatu kwa haraka sana. Sifa zote ziende kwake.

7. Aucho leo hakuonekana, ni kama hakucheza kabisa kwenye mechi. Kipindi cha kwanza nilidhani alikuwa akiusoma mchezo ila baadaye nikagundua aliweza kuzidiwa kimaarifa pale katikati.

8. MANURA...Yaani kama golikipa alikuwa akiruhusiwa kwenda uwanjani na kiti, gazeti ili asome, basi leo Manula alitakiwa kufanya hivyo, ukiachana na ile off target ya Mayele, hakuna nyingine yoyote iliyokwenda langoni mwake. Inonga na Onyango walimlinda sana kiasi cha kutokufikiwa kabisa.

9. Leo nimeshuhudia jinsi kocha Pablo alivyoweza kuwazidi kimbinu makocha wawili, Nabi na Kaze. Alianzisha mashambulizi kuanzia nyuma kabisa, Yanga walivyokuwa wakivutika, zilikuwa zinapigwa kaunta attack kwa Morisson ambaye aliwaadhibu kwa mabao yake mawili safi kabisa.

10. KIBU ni mtu na nusu. Bao lake moja alilofunga inaonyesha kabisa kwamba ameimarika mno. Kasi yake ilikuwa ikiwachanganya sana mabeki wa pembeni wa Yanga kiasi cha kuhisi jamaa alikuwa na mapafu ya mbwa.

NB: LEO NDIYO TUMEGUNDUA KWELI ALIKUWA AKIIHUJUMU TIMU.

Imeandikwa na Nyemo Chilongani.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Bangi ya kuvutia chooni ni mbaya sana upelekea watu kuwa vichaa bila familia kutambua ndugu yao ni kitu gani kimemkuta!
 
Ujinga mwingine wote ungesameheka lakini Manula kuwa likizo hapana.
 
Ndoto za alinacha hizi. Yaan wale wazee wa simba ndo wawafiche kina fei toto, bangala na aucho
 
Nakuhakikishia kua Morrison hata perfom. Every one knows his moves and tactics.
 
Ugoro na milungi ya Buguruni hiyo.Pole sana
 
sawa Kabwili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…