Mwalimu wetu wa kwaya alizimia kwa kufunga

Hawa waalimu wa kwaya kwa kutafuna waimbaji wao hawajambo,pengine alikuwa anatafuta kusifiwa na mabinti katika kwaya ili awatafune vizuri....
 
Mwambieni mwalimu wenu wa kwaya ni sunnah kula daku.
 
Yesu pekee ndie alieweza kufunga siku 40 bila kula. Asirudie tena huyo atakufa ingawa lengo lake ni zuri

Ukiwa msomaji wa kiutafiti katika kuyachunguza maandiko utagundua pia hakuna aliewahi kufunga 40 pasipo uwepo wa Mungu, Lazima Mungu awepo ndo unaweza kufanya hicho kitu na istoshe sio hiari ukiangalia Musa alifunga 40 Mara tatu mfululizo lakini ni kwamba katika hizo tatu, mbili haikuwa choice yake ila ilikuja by the way au naweza sema by circumstances au tuseme hakupenda au hakupanga. kwani alipokwenda mlimani kuchukua amri hakuambiwa afunge 40 ila kinachoonekana ni kwamba Mungu alikaa kimya mpaka akajikuta amekaa hizo siku 40 au alifundishwa hizo amri kwa siku 40. Aliposhuka chini akakuta watu wake wamejiharibu nafsi na kwa vile alishuka na nguvu ya upako na uwepo wa Mungu kutoka mlimani aliweza kustahimili 40 nyingine ili kuwaombea toba. na hata aliporudi mlimani hakusema nakaa 40 tena ila ni mazingira yaleyale ya awari ndo yaliyojiri. kadhalika Nabii Elia alikua anamkimbia mwanamke kwenda kule mlima wa Mungu sinai. pia tunaona Mungu alimtokea kule na ni wazi kwamba hakupanga kufunga siku 40 ila ilijikuja by the way na pia kumbuka aliletewa chakula kabla ya huko kufunga kwake aliletewa na malaika chakula kutoka juu. pia hata Bwana wetu Yesu Kristo hakusema anaenda kufunga siku 40 au biblia haikusema Yesu aliongozwa kwenda kufunga, hapana ila inasema ilongozwa kwenda jangawani HATA baada ya siku 40 aliona njaa. kwa hiyo alipoongozwa na Roho kwenda jangwani very likely pia hata yeye hakuambiwa afunge ila kwa vile Roho alimuongoza kwenda jangwani (kiufunuo jangwani ni mahali ambapo mahitaji ya mwili wa nyama hayapatikani) na pia nionavyo Roho baada ya kumfikisha huko jangwani alimtelekeza huko jangwani pasipo chakula wala maji. na hii ilikua kwa sababu aweze kujustifiy kutukomboa kutoka katika nguvu ya majaribu ili kwamba pasiwe na jaribu ambalo linaloweza kuvuka hapo kwa maana kwamba kila pigo tutakalopitishwa maana yake hiyo dhiki haitafikia kipimo cha funga ya 40 na kwa maana hayo majaribu yote pia yatakua yameshindwa juu yetu kwa kuwa Bwana Yesu kwa kwenda kwenye kipimo cha juu cha majaribu kwa njia hiyo tumeshindiwa mapigo yetu wala sio dhambi peke yake pia na nguvu ya kushinda majaribu magumu.
 
David Brain alifunga siku 48 pia, tena alikaa kwenye box la vioo lililoning'inizwa mtaani ili watu waone ni kweli hali kitu kwa siku zote hizo, Jesus huenda alikuwa anajitengenezea mikate anatupia mara mojamoja.

Kaka Yesu sio mbinafsi: alisema hivi

Mkiniamini kazi nizifanyazo nanyi mtazifanya- Naam na kubwa kuliko hio mtazifanya.


kwa hiyo tutapopata neema ya kufanya jambo kubwa kuliko alilofanya Yesu tusijisifu kwamba tumemzidi ni kwamba ametupenda na kutuwezesha kufanya zaidi ya yale aliofanya yeye binfsi
 
Jamani lazima tuangalie kufunga hakumlazimishi Mungu kujibu maombi yako.Kufunga ni ishara ya unyenyekevu utii naitlivulivu.Kuna kufunga kwa nafsi au mwili au roho.Pia kuna kufunga juu ya vitu unavyovipenda au vilivyokamata nafsi yako yaani vinavyotamanisha!!Na lazima tuelewe ni kufunga na kuomba na sio kufunga tu.Pole mwalimu wa kwaya kwani si kawaida yenu kufunga
 

sina neno
 
Kama wewe ni mwanafunzi wake, kwa hilo jina lako asingeacha kuanguka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…