Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 70,916
- 141,437
Baada ya kukumbuka lile tukio la kufukuzwa, japo sio ishu saaana nimeona niwasimulie na huyu mwamba sasa alietunyoosha mimi na dada angu na huu ndio ukawa mwisho wa outing. Yaani outing zikawa za moto hakuna alietaka kusikia mtoko tena.
Nicheke tu kwanza! Haya mambo yote yalikua ni harakati za usichanani huko, kwetu tupo wakike wawili japo kanizidi kidogo ila hizi harakati za kijinga tulikuaga bega kwa bega na ni mambo yaliyotokea miaka ya nyuma huko jamani msimind sana 😁, sasa hivi sisi ni watu wazima wamama na familia zetu tuna watoto wa kutosha, hivo hizi harakati ni zilipendwa sisi wenyewe tukikaa kukumbushiana ni vicheko tu vinatalawa.
Dj nisindikize na amekoma side mnyamwezi😁. Enzi zile zile za kufukuzwa , siku moja jpili nimetoka kusalimia ndugu mitaa ya ilemela kule natembea sasa nikapande gari kurudi home nyuma yangu ikawa inapita rav 4 ya maroon akashusha vioo haujambo binti, twende nikusogeze nikazuga zuga bado natembea akarudia tena twende nikusogeze usijali nami naelekea huko nikaona isiwe shida ngoja nisipigwe vumbi hapa chap nikafungua mlango nikazama ndani, story zikaanza salamu unaitwa nani unaenda wapi huku ulikua wapi, akasema nlikua na ishu zangu hapa ila ngoja nikupeleke akanifikisha hadi mitaa ya nyuma nyuma kidogo nikamwambia niache hapa nitafika home akatoa noti noti akanipa na namba akaniandikia kwa karatasi sikua na simu mie.
Kesho yake sasa Monday, naenda skonga nimejaa 😁, nimekaa kwenye desk nikatoa moja nikampa nliekua nimekaa nae akauliza leo una hela nyingi umetoa wapi nikamsimulia, akaguna mmmhh sikumpa details story tu general kwamba nilikutana na mtu mitaa flani akanipa lift, yeye akasema dah huyo jamaa ana rav 4 ya maroon, nikajibu ndio, mrefu mweusi anaitwa flani mie ndio akacheka nkaona mmmh🤔🤔 akasema jamaa muhuni sana sketi haipiti na inasemekana ana ngoma. Nikaona hapa mambo yashapandiana mapema sana😁
Zimepita siku kadhaa nikamuona mitaa ya home anasimamia ujenzi wa hotel flani, basi kila nikipita ananipa vihela akiomba mtoko naruka ruka, akaona nampotezea muda tu. Siku moja sista kapita akamuona akaanza kufatilia akampa namba akampa na hela basi kujifanya ana akili sista akapewa namba ya tigo mie voda kumbe sisi huwa tunasimuliana tena ukiwa ni mtu tunamchukulia poa tu hamna mwenye mpango nae. Sisi akawa ananipa story sasa nimekutana na lijamaa limenipa hela bla bla ila character ni za yule akamdanganya na jina mi nikamwambia mbona huyo mtu ndio alienipa mie hela 🤣🤣🤣 tukacheka tu.....