Mwamba ametusaliti wana Simba, Karma haitakuacha salama

Simba lunyasi

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2022
Posts
385
Reaction score
840
Kusema ukweli huyu mchezaji alikuwa ndio kipenzi cha wana Simba, yaani mwamba tulikupenda sana lakini ndio hivyo tena.
Tulikupa ufalme wa soka la nchi hii, tukakuimba na kulitaja jina lako kila mahali..

Kati ya timu zote duniani umekosa timu ya kwenda paka kuamua kwenda kwa hawa maadui zetu utopolo??

Sisi sio pipozi tutakutana...........
 
Si mlishangilia Fei kwenda Azam? Mkisema kama mchezaji akipata malisho mazuri aruhusiwe kuondoka? basi huyu kapata malisho mzuri zaidi. Pia usianze kusema ni karma kumbe mna mpango wa kwenda kumloga.
 
Kaka uko too primitive. Hakuna usaliti wowote ni maamuzi yake. Wachezaji kibao tu wanahama timu zao ulaya, tena major players na watu hawalaani, grow up. Watakuja wachezaji wengine wataziba hiyo nafasi
 
Kinacho huzunisha zaidi kuhusu usaliti ni kwamba usaliti huwa hautoki kwa maadui zako ; una toka kwa watu unao waamini zaidi .

Simba ni kubwa kuliko chama . Tuendelee kuipenda Simba , mnyama mkali mwituni, mfalme wa nyika .
 
Inatosha walishauza mechi acha aende huko wachezaji bado wapo bhana
 
Nikabubujikwa na machozi sana
 
Usaliti upo wapi hapo na mwamba katupa kila kitu wana Simba? Acha akachukue pesa huku hakuna kipya atakachotupa zaidi ya kuzuia damu mpya kuonyesha uwezo.
 
Chama amekwenda Yanga kwa vile mkataba wake kuichezea Simba umekwisha , na Simba haikuwa na matumizi naye tena ndiyo maana amekwenda Yanga hajaisaliti Simba hata kidogo. Kama Simba wangekuwa wanamuhitaji asingekwenda Yanga, na wewe mleta uzi siyo mwana Simba, sisi wana Simba wote tumefurahi Chama kuondoka na tunamtakia maisha mema huko aliko.
 
Karma huwa haifanyi kazi kwenye vitu vya hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…