Mwamba wa Hiphop halisi, Saigon 'Treach' wa iliyokuwa D.P.T ana masahibu gani hivi?

Mwamba wa Hiphop halisi, Saigon 'Treach' wa iliyokuwa D.P.T ana masahibu gani hivi?

funluverx

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2014
Posts
480
Reaction score
343
Huyu ni Saleh, almaarufu 'Saigon'.
Mwanachama wa-miongoni mwa makundi ya awali kabisa kuwahi kutamba katika tasnia ya muziki wa Hiphop.
Hapa tunazungumzia mwanzoni kabisa mwa miaka ya 90.

Jamaa alikuwa Mkali kwa kwa maana halisi ya ukali kuanzia katika Tungo na Style yake.
Si hivyo tu Mchizi kunako 'tambo huru', moja ya nguzo muhimu na za lazima za Hiphop, yupo vizuri.

Sanjari na sifa hizo huyu bwana amejaaliwa 'Yai' ambalo ukiwaondoa pengine aliokuwa akifukuzana nao kwa karibu enzi hiz,
watu kama akina Eazy-B au D-Rob wa KU crew, Saigon hakuna wa kufanana nae hadi sasa na pengine hatatokea.

Nilifurahi wakati fulani pale alipoweza kuonyesha kipaji na uwezo wake mwingine katika maswala ya utangazaji hasa kwenye Runinga. Nani hakumbuki kionjo chake kilichotamba cha 'Ebwana Dah!' wakati ule akiwa na EATV?

Nikaja kumuona mara kadhaa akionekana mpenzi wa Kanzu, Bargashia wakati mwingine full-Hagal,
Tofauti na mazoea yake ya uvaaji wa ki-hiphop haswaa, pensi, T-shirt, Boots, Sneaker nk.
Kuuliza naambiwa jamaa sasahivi swala haimpiti. -Nikasema safi.

Mara kapotea, hainekani wala hasikiki tena.

Hoja ya uzi wangu;
Huyu bwana nimemuona wiki ya jana maeneo ya Sinza,
Siha na muonekano kwa kumuangalia tu, -Kuna shida,-Hayuko sawa.

Ndugu, jamaa na marafiki mnaomtakia mema huyu mwamba mtafutena angalieni mnamsaidiaje.

Na kama yupo anaejua anasumbuliwa na nini si mbaya kutumegea.
 
Lakini as long as tuna dizasta vina hakuna kilicho haribika pengo lake limezibika vizuri bila kuacha space
 
Hakika jamaa ana kipaji na akili.
Mpaka mwishoni mwaka jana alikuwa akitangaza Tv na Radio Iman, huku akionekana full kiustadh. Kwani aliacha hiyo kazi?
 
Back
Top Bottom