Mwambieni Pep Guadiola haya machache kuhusu EPL

Hahahaha halafu pep inaonekana hajui kuua gem nje ya uwanja hana ile mikwara ya morinyo, fergie, kabla yagem
Na ndio itakuwa sumu yake. Mou na Fergie wanacheza kwanza kwenye vyombo vya habari kabla ya siku ya game. Maskini Pep mambo hayo hana. Nakumbuka kuna kipindi Fergie aligoma kuhojiwa na BBC kwa miaka kadhaa sababu hio hio ya kupenda kucheza game kabla ya siku yenyewe
 
Fergie, Mou na Benitez ndo wanaijua hiyo ligi vizuri. Makocha wengine wanaonewa tu maskini. Bahati mbaya sana Benitez kajipoteza kiaina
Weeeeeee ndio umepotea na si benitez
wale jamaa wanavyoipa promo epl na championship huwezi sema benitez kapotea
 
Wenger haongezi mkataba na huu ndio msimu wake wa mwisho...
alishindwa chukua mbele ya leicester ataweza sasa ivi
 
Wenger ni overrated. Uwezi kumuweka kwenye levo moja na Pep au Mourinho. Makocha waliochukua makombe ya kila aina wakati yeye hana kombe lolote la Ulaya.
Wenger sio overrated bali alikuwa anafanya kazi kulingana na ukubwa wa kikosi chake, sasa we ulitaka abebe kombe la uefa kwa kushindana na team kama barca, madrid, juve, man u, chelsea, bayern au psg? Acha unafki kwa muda mrefu sana wenger amekuwa na kikosi ambacho hakiwezi kushinda mataji makubwa, na ndiomaana kipindi kile miaka ya 2004-2006 alifika fainali ya uefa kwakuwa alikuwa na kikosi cha wachezaji wazuri

Baada ya hapo ye alichokuwa anafanya ni kuhakikisha anafanya biashara ya kuingiza hela ili walipe deni la kujenga uwanja na baada ya hapo ndio kaanza kununua wachezaji ghari kama kina sanchez, ozil, xhaka, mustafi na wengine, sasa ukisema eti wenger ni overrated sikuelewi labda kama we unaijua maana tofauti ya hilo neno

Kwa ligi ya England sio swala la kubeza kwa wenger kumaliza kila msimu top four ikiwa makocha kibao wao wameshindwa, na amekuwa akifanya hivi kila mwaka ili tu apate hela za uefa ili afikie lengo la club
 
Ubishi mwingine buana.....haya ongea kuhusu 'ughali' wa kikosi cha Leicester kilichobeba EPL
 
Ubishi mwingine buana.....haya ongea kuhusu 'ughali' wa kikosi cha Leicester kilichobeba EPL
Acha ubishi wa kijinga kwahiyo kushinda kwa Leicester ligi ndo kunafanya wenger awe overrated? Kwani wakati Leicester wanashinda ligi hao makocha ambao sio overrated kina mou walikuwa wapi? Sometimes kushinda taji ni bahati tu kama ilivokuwa kwa Chelsea na dimateo kwenda kushinda uefa ila sio kweli kwamba walikuwa bora kuliko team zingine

Aina ya ushindaji wa kombe kwa Leicester ni kutokana na team pinzani kwanza kuwadharau na pia wao kuwa na spirit ya ushindi mwanzo wa ligi hadi mwisho wa ligi, na kuna team zimewahi kufanya hvo kama Blackburn, Aston Villa, Newcastle, ila sio kusema eti Leicester walikuwa wazuri kuliko Chelsea, man city au arsenal ila upepo tu ulikuwa wao
 

Kweli mashabiki wa Arsenal ni vihiyo. Atletico Madrid wana bajeti ndogo zaidi ya Arsenal ma wana kikosi kidogo zaidi ya Arsenal lakini wameingia fainali mara mbili ndani ya miaka mitatu. Uyo Mzee wenu yeye anaishia 16 bora miaka nenda rudi,anamaliza nafasi ya 4 akijitahidi sana anamaliza ya 3/2. Wenger ni Overrated. Period
 
Ndio maana hadi leo hii Arsenal wana mashabiki. Wengi wenu ni vihiyo.
 
Hebu nambie kwanini unasema wenger ni overrated? Tuanzie hapo kwanza maana mada haihusiani na wenger
 
Umesahau kumwambia kuwa Granada na Levante wakija EPL hawatabanduka kwenye top four kama sio kuchukua ndoo....!

Mwambie kuwa La liga ni ligi bora kuliko EPL

Mwambie kuwa La liga imedominate soka la Ulaya kwa miaka 10 mfululizo, Champions League na Europa League

Pia mwambie Real Madrid ndio club tajiri kuliko zote dunian

Mwambie kuwa Barcelona yake ilikuwa tishio haijawahi tokea katika ulimwengu wa soka tuka dunia imeumwa

Mwambie pia, alimtetemesha Fargie na EPL yote

Mwambie pia, Messi wake alimtwanga 4 Wenger

Mwambie EPL ni internal league, nje ya hapo, wanapigwa hata na vitimu vya mtaani huko Slovakia
 
Mm siku zote najua soka la Mou ni la kihuni sana. Nakumbuka mara ya kwanza kutua la liga pep na barca yao wakampiga bao 6, lakini mwisho wa siku Pep kakimbia ligi shauri ya Mou. Na ndo maana namuonea huruma Conte na Chelsea yake
nakumbuka sana kipindi hicho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…