Mwambieni Rais Samia Suluhu Hassan

Mwambieni Rais Samia Suluhu Hassan

Corticopontine

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2019
Posts
666
Reaction score
1,277
Katika muendelezo wa Samia kushindwa kuiongoza nchi yetu kwa uwezo wake akina zitto wanamshauri kuwa ili afanikiwe ni kuhakikisha legacy ya Magufuli inafutika kabisa. Na kwa akili yake anadhani hilo linawezekana! Its never kuifuta image ya Magufuli Tanzania madam president wanakudanganya! Magufuli ni hero wa Karne.

Samia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jemedari Magufuli anajifanya kufumba macho yani kama haoni vile namna akina zitto na baadhi ya wanaCCM wenzake wanavyokesha kwenye mitandao kumdhihaki aliyempendelea kumteua awe makamu wa Rais. Hata siku moja Samia ameshindwa kufungua mdomo wake kulaani na kukemea udhalimu huu kwa aliyekuwa Rais wa Taifa letu aliyeweka rehani maisha yake kwa ajili ya nchi yetu.

Mlio karibu na Samia mwambieni what goes around comes around, yeye anadhani akikaa kimya wakati magufuli anadhihakiwa akiwa mapumziko yake ya milele yeye atakuwa salama baada ya kumalizi muda wake au kutangulia naye mbele za haki. Mwambieni asijidanganye kamwe.

Mbaya zaidi wapambe wa Samia wanamjaza kwenye kumi na nane kwa kumlinganisha kiutendaji na Magufuli, daaaaah come on guys! Kweli hii dunia ina watu waliokosa hata chembe ya haya! Samia muigiza muvi mnamlinganisha na Magufuli The Reformer! Mungu atawachoma Jehanamu trust me.

Mkumbusheni samia kuwa anajua fika huyu Magufuli anayeacha adhihakiwe ndiye aliyefanya kwa nguvu zote hadi viti anavyokalia pale Ikulu ya Chamwino vinunuliwe baada ya kuzuia ufisadi na rushwa iliyokithiri ya watu kwenda kusainiana mikataba ya rasilimali zetu kwenye vyumba vya hoteli.

Mkumbusheni Samia yafuatayo labda atanzinduka tafadhali;

1. Ile Ikulu ya Chamwino anayokaa kwa raha zote ilikuaga ni set up ya baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na iliwashinda marais wote baada ya Nyerere na walikuwa hata hawakai hapo walikimbilia Dar. Lakini chuma JPM aliwatumia vijana wa Taifa letu JKT wakaijenga usiku na mchana kwa jasho na damu na uchungu kwa Taifa lao.

2. Msiogope mkumbusheni samia atoke usingizini kuwa zile ndege anazopanda kila siku kupigia misele na kwenda kuigizia muvi ambazo akina zitto wameanza kumshauri asizipande ili kuifuta legacy ya JPM aliyezinunua tena kwa mbinde akiwa anapingwa kila kona na haohao ni Magufuli. Mshitueni mama enu kuwa hadi Kikwete anatoka madarakani Taifa halikuwa na ndege hata moja.

3. Muamsheni samia atoke usingizini na mmwambie huyu Magufuli anayefumbia macho kudhihakiwa kwake akiwa kajipumzikia ndiye aliyeanzisha miradi yote ya kimkakati ambayo kuna kila dalili ya yeye kushindwa kuiendeleza na badala yake ameanzisha mradi wa kuigiza muvi.

Mwambieni Samia ukimya wake ndiyo unaotupa mashaka juu ya kifo cha Rais wetu na ndiyo maana watanzania tunataka

THOROUGH, CREDIBLE AND TRANSPARENT INVESTIGATION juu ya kifo cha ghafla cha Magufuli wetu.

R. I. P JPM
 
Nje ya mada
IMG-20220504-WA0272.jpg
 
Tatizo lenu mlijimilikisha hii nchi kama yenu peke yenu..mkafanya watu waishi kwa hofu na uoga..mkajichotea mipesa kimyakimya kwa gia ya kusaidia wanyonge..mkakopa na kukopa tena huku mkidanganya mnajenga miradi kwa fedha za ndani kumbe mnakopa kwa siri..leo mama kila anachofanya anaweka hadharani imekua nongwa.?
 
Back
Top Bottom