Mwambieni Rais Samia Suluhu Hassan

Mwambieni kabisa afanye kazi Mara Mbili ya JPM ndipo kidoogo ataeleweka.
Sasa kama robo yake kashindwa mbili ataiweza. Kwa sasa tunajivunia kukopa kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo vya shule huku tukijilinganisha na wamarekani.

Mama hajatuambia pia alivyokutana na vyoo vya covid 19 marekani.
 
Alifanya kazi gani huyo mtu

Maana miradi yote ya Flyover ni awamu ya JK na Mwendokasi

Yeye alibuni kitu gani kipya?

Amekopa mpaka tumebaki vuuu........ ziiii
Huyu huyu JK ambaye alikuwa payrol ya wafanyakazi wa serikali ilikuwa kwa bakhresa au unamzungumzia JK yupi? Huyu aliyekuwa anakopa exim bank mishahara ya kulipa wafanyakazi.
 
Wakati JK anaondoka hiyo miradi ilikuwa imefikia hatua gani?
JK aliacha terminal 3 ikiwa imesimama na mkandarasi akiwa ameshalipwa pesa yote ya mkopo..huo ndio mradi aliyoacha, mengineyo yalikuwa kwenye makaratasi tu kama nyerere alivyoacha dodoma capital na stieglers kwenye makaratasi.
 
Ukienda hospitali za serikali leo ndiyo utaona tofauti kubwa iliyopo kati ya sasa na 17.3.2021 backward
Au tembelea insta akaunti uone tofauti ya miradi ya afya 17.03.21 backward na baada ya 17.03.21 ahead.
 
Umkumbushe samua pia zike biluoni 71 zilizopelekwa mwanza kutoka bandari dar ziko chatoooooo
 
Nikajua umeandika vya maana kumbe takataka.
 
Zaidi ya kitambulisho cha machinga huyo mwendazake hakua na jipya.alikua anaingilia petty issues kama vyoo vya stendi,Masoko,branch za bank ambavyo havikuwa hata kwenye level ya uraisi
Nacho ndio mpaka ununue ,saizi huo upuuzi hakuna.
 
SGR, NYERERE HYDROPOWER, NJI WA DODOMA NK
Sgr inatumika au aliishia kuweka Jiwe la msingi tuu?

Nyerere hydropawa inazalisha umeme au aliishia kuweka Jiwe la msingi?

Dodoma- imefanya nini? Mji si ilikuwepo na wewe umezaliwa umeukuta au kuna jipya?
 
Au tembelea insta akaunti uone tofauti ya miradi ya afya 17.03.21 backward na baada ya 17.03.21 ahead.
Miradi ya afya ni jambo moja na ubora wa huduma za afya ni jambo jingine
 
Nchi inaendeshwa vizuri kabisa na mama, wewe unakuja na sumu ya eti "kushindwa". Nini alichoshinwa Mama Samia Suluhu Kukiendesha?

Mama kwa mwaka wake mmoja tu kapiga hatua amabyo Magufuli hajapatapo kabsa kuiifanya kabisa mwaka wake mmoja.

Wacheni kujazana ujinga, tunafahamu chuki zetu ni Uislam tu, hakuna zaidi.
 
Tofauti ipi hiyo ikiwa chanjo tuu za watoto hazikuwepo ukiachilia mbali condom 😁😁
Mgonjwa anapokelewa lakini urasimu wa kumhudumia mpaka uwavute watu pembeni nadhani umenielewa na kama huna kitambi au suti hata huyo wa kumvuta unaweza usimwone
 
Kazi kama zipi alizochapa ambazo wewe zilikutoa kwenye umaskini?

Huyo ndio alizalisha maelfu ya maskini kwa kuitwa machinga na hakuwa anaajiriπŸ‘‡

 
Mgonjwa anapokelewa lakini urasimu wa kumhudumia mpaka uwavute watu pembeni nadhani umenielewa na kama huna kitambi au suti hata huyo wa kumvuta unaweza usimwone
Uwavute wakina nani hiyo pembeni? Tangu lini hospital kuna huduma za bure?

Miaka yote iko hivyo sio tuu huko hospital ila hadi Polisi,mahakamani nk..

Huna pesa Kaa kwenye foleni.Kwanza wenye pesa hawaendi hospital za umma unless ni kwenye specialised treatment..

Pili kama hospital za umma ni mbaya kwa kiasi hicho kwa nini watu waende kurundikana huko? Si waende private sasa kwa sababu kule mpaka uwavute watu pembeni? πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…