Uchaguzi 2020 Mwamkulu Mpanda: Mtia nia wa Udiwani almanusura apoteze fahamu baada ya kuanguka ghafla wakati kura zikihesabiwa

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mtia nia Udiwani katika Kata ya Mwamkulu iliyopo Manispaa ya Mpanda ambaye amepata kura 5 nusura apoteze fahamu baada ya kuanguka ghafla alipokuwa akitazama karatasi za kura za Mtiania Kalip Katani anaye tetea Udiwani.

Mtia nia huyo ameishiwa nguvu wakati anaona karatasi nyingi zina muelekea Kalip Katani . Mpaka dakika ya mwisho Kalipi Katani amepata Kura 69 kati ya kura 75 halali kutoka kwa wajumbe akifuatia na Mtia nia aliyepata kura 5 mwingine akijizolea kura 1.

Your browser is not able to display this video.
 
Hawa jamaa kama wanataka mali wataipata Shambani
 
Watakuja kufa hawa, wanajiingiza kwenye mambo ambayo hawawezi kuyahimili
 
Siasa itakua roho ngumu sana, kama huna acha utakufa siku si zako.
 
Alisikia kelele za mitaani alipoitwa "diwani, diwani" kila alipopita akajihesabia tayari ashaula.
Usicheze na wajumbe Mr.
 
Huyu naona katumia Hela kuhonga

Ova
 
Mtindo ulioanzishwa wa kuhesabu Kura hadharani ni mzuri sana Ila ulitakiwa uanze kutumikia kumchagua mgombea urais kupitia chama tawala majina yakiwa zaidi ya moja au wanachama wakiwa wengi waliogombea nafasi hiyo, pili mtindo huo unatakiwa utumike kwa uchaguzi mkuu wa October mwaka huu.
 
Nimechekaaaa
Watia nia ni kweli mnania ya kuwatetea wananchi au kuna lingine maana si kwa kupanic huku! kaaah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…