Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 34,020
- 79,098
Katika kilichoonekana kama kusogeza ‘huduma’ karibu kwa waumini wa kanisa lake, Askofu na Mtume Boniface Mwamposa yupo kwenye mchakato wa kuinunua EFM Company Limited.
EFM ni kampuni iliyosajiliwa kama chombo cha habari, ikiwa na umiliki wa Redio na Televisheni.
Mwamposa na Mkurugenzi wameshibana…
Mkurugenzi wa EFM Bwana Francis Ciza maarufu kama Majizzo (Mume wa muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’) wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na Askofu Mwamposa katika kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mikutano na ibada zinazoendeshwa na Mwamposa kwa kipindi kirefu.
Baada ya kufanya kazi pamoja kwa kipindi kirefu, hivi sasa wapo kwenye mazungumzo ya kumuuzia media hiyo Mwamposa.
Nimetaarifiwa kwamba vikao vya mauziano hayo vinafanyika kwa siri nyumbani kwa Majizzo, huku dau likiwa bado halifahamiki lakini ikielezwa Majizzo anataka dau kubwa linalokwamisha taratibu za mauziano kuanza.
EFM Radio imemshinda Majizzo!
Kwa kipindi kirefu kumekuwa na minong’ono ya wafanyakazi kushindwa kulipwa mishahara kwa wakati, ikisemekana wanaolipwa bila kusumbuliwa ni wale watangazaji wenye majina makubwa pekee, huku wale wachanga wakipitia wakati mgumu kimalipo.
Taarifa za uhakika ni kwamba redio hiyo imemshinda Majizzo, changamoto za uendeshaji zimemuelemea na inasemekana kama sababu kuu ya yeye kufikia uamuzi wa kumuuzia Mwamposa kampuni yote hiyo ya habari iliyokuja kuzipa chachu redio kongwe miaka ya mwanzoni mwa uzinduzi wake.
Majizzo siye mmiliki pekee…
Taarifa za usajili wa kampuni zinaonesha kumilikiwa na ndugu watatu, yeye Majizzo (Francis Ciza 40%) ndugu zake kwa upande wa baba yake mlezi Mzee Ciza… Jean Ciza 40% pamoja na Justine Ciza 20%
Wenu katika unyetishaji, mimi na chanzo changu,
Nifah.