Mwana FA hajui mnyororo wa thamani katika sherehe za harusi, aelimishwe...

Kuna mambo mengine kwenye jamii hayaepukiki moja wapo ni hili la kuchangia mambo ya kijamii.
 
Bora hiyo harusi ifanyikie hapo inafanyikia mbaaaliiiiii nauli ya kwenda kurudi malazi, unanunua ng'ombe
 
Kuna mambo mengine kwenye jamii hayaepukiki moja wapo ni hili la kuchangia mambo ya kijamii.
Sio harusi, showers, birthday maana siku hizi hadi vipaimara tunaletewa kadi..hii jamii imekujankuwaje ... Yaaani mtoto aende mafundisho miezi 6-8 usijipange uje uchangishe watu !!??
 
Haikupi raha kuona mchango wako unatoa ajira kwa watu?
Toka hapo ulipo nenda kanuunue nguo duiani, kanunue maredio na ma tv na Kodi bodaboda zunguka mji wote utasaidia watu kupata ajira ati.
 
Kuhusu kuhusisha mchango na ajira naona umepotoka...Mwana fa alisisitiza ishu ya maandalizi kwa mlengwa mwenyewe. Hilo haliondoi watu kupata ajira kama unavyotaka.Mf. Kama harusi yako ni milioni kumi,muoaji jichange mwenyewe upate milioni kumi (ajira ulitotaja zitapatikana)...Hata watu wakikuchangia itakuwa milioni kumi (ajira ulizotaja zitapatikana) huo ndio nadhani mtazamo sahihi. Labda kama unataka harusi ya mil.10 wewe unayo laki mbili….unataka michango ndio ijazie hapo kweli tutafeli; na ndio wengi wanataka hiyo kitonga Mtizamo
 
Kwa point zako bado Hamisi yupo sahihi...kuna njia nyingi za kudumbukiza hela zako kwenye mzunguko...kafanye hata shopping kwa machingaz
 
Nakubaliana na MwanaFA, ajira sio lazima utegemee michango yetu. Hebu tupumzisheni, hapa Nina kadi za ndoa sita harusi kabla ya xmas ambazo naona moja ndio labda watavuka miaka mitano.

Hebu niacheni sichangi hata moja BTW yangu nikibahatika kaurithi na pesa yangu flani nikapiga bila kuchangisha 13 years ago sitaki usumbufu kwa sasa kila mtu apambane na mkewe.

Imagine juzi natumiwa msg sasa Hadi kipaimara watu eti wanachangisha huu upuuzi zamani haikuwepo, mzee alikuwa anajipanga anapigansherehe mwenyewe anaalika watu wake kadhaa mnapiga kipaimara Mambo kwisha.

Huu utaratibu wa michango uwepo kwa vijana wenye projects zilizosimama na wakiwa wanataka funds zaidi au kusoma (elimu) , hospital (maradhi) Ila starehe yenu chumbani siwezi kuichangia No thank you.
 
Sherehe sio lazima mkuu. Anaweza funga ndoa vizuri kabisa bila ya sherehe kama uwezo ni mdogo.
Nendeni kanisani barikini ndoa Kisha nendeni kwenu kale ugali dagaa siku inakwisha.

Msiwatafutie watu shida kwa matatizo yenu ya kuchonga
 
Mkuu unatetea michango sababu yako iko karibu sio? 😄
 
Nitachangia msiba na maradhi tu kwa sababu sio utashi binafsi wa mhusika.Vinatokea tu havipangwi.
Arusi upange mwenyewe halafu gharama nichangie?Ni ujinga ambao sitafanya hata siku moja.Sijachangiwa wala sichangii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…