Mwana FA: Serikali Itasaidia Kutafuta Wadhamini Michuano ya Bahati Ndingo CUP

Mwana FA: Serikali Itasaidia Kutafuta Wadhamini Michuano ya Bahati Ndingo CUP

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Naibu Waziri Wa Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe. Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) amesema serikali kupitia Wizara yao itasaidia kutafuta wadhamini kwenye michuano ya Bahati Ndingo CUP 2024, iliyoanzishwa na Mbunge wa Jimbo la Mbarali, ili kuongeza zawadi Kwa washindi kwakuwa michezo ni ajira.

Mhe. Mwinjuma alisema hayo baada ya kushuhudia fainali ya mashindano ya ligi ya Mbunge wa Mbarali, Mhe. Bahati Keneth Ndigo, mchezo uliozikutanisha timu za Ubaruku na Madibira kwenye uwanja wa Highland Estates, wilayani Mbarali, Mbeya, tarehe 12 Novemba 2024.

Katika mchezo huo, timu ya Ubaruku ilishinda na kutangazwa mabingwa baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati, kufuatia mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1.

Mwinjuma ameeleza wakati akihitimisha michuano hiyo ya Bahati Ndingo CUP 2024, kwenye fainali iliyo zikutanisha timu za Kata ya Madibila na Ubaruku kwenye Uwanja wa Highland Estate wilayani Mbarali na timu ya Kata ya Ubaruku kuibuka washindi Kwa mikwaju ya penati baada ya timu hizo kutoshana nguvu ndani ya dakika 90 Kwa kufungana bai Moja kwa Moja, na kuondoka na kitita cha shilingi Millioni 5 na kikombe cha ubingwa.

Michuano hiyo iliyoanzishwa Kwa mara ya kwanza mwaka huu wilayani humo imezikutanisha Timu zaidi ya 20 kwenye Kata za Jimbo la Mbarali ambapo mshindi wa kwanza amepata shilingi millioni 5, Mshindi wa pili akipata milioni 3 na Mshindi watatu millioni 1 pamoja na zawadi Kwa timu yenye Nidhamu, mchezaji Bora, mfungaji Bora na golikipa Bora.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Mhe. Bahati Kenneth Ndingo amesema kuwa tumehitimisha ligi ya Bahati Ndingo CUP 2024 wilayani Mbarali, katika viwanja vya Highland Estate kati ya Ubaruku Vs Madibira na Tunashukuru sana Mhe Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma kwa heshima kubwa aliyotupatia wanambarali

Screenshot 2024-11-13 at 20-02-11 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-11-13 at 20-02-20 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-11-13 at 20-02-24 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-11-13 at 20-02-28 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
 

Attachments

  • Screenshot 2024-11-13 at 20-02-15 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-11-13 at 20-02-15 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    846.2 KB · Views: 5
  • Screenshot 2024-11-13 at 20-32-36 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-11-13 at 20-32-36 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    871.8 KB · Views: 6
  • Screenshot 2024-11-13 at 20-28-00 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-11-13 at 20-28-00 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    706.7 KB · Views: 5
  • Screenshot 2024-11-13 at 20-24-27 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-11-13 at 20-24-27 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    623.8 KB · Views: 6
  • Screenshot 2024-11-13 at 20-25-05 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-11-13 at 20-25-05 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    799.7 KB · Views: 5
  • Screenshot 2024-11-13 at 20-25-21 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-11-13 at 20-25-21 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    952.3 KB · Views: 6
Back
Top Bottom