Mwana FA ulioanza nao game wamekutenga, kuna sehemu umekosea au tatizo nini?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari wadau,

Mimi mshabiki sana wa Bongo Flavour na nafurahi sana kuona wasanii waliokuwa pamoja wanazeeka pamoja kama marafiki au hata jamaa japo maisha yanatutenganisha.

MwanaFA na Sugu mmekaa pamoja gheto majuu enzi hizo.. Nilionaga picha mpo pamoja..

Kipindi kile Sugu anapambana na unyonyaji Clouds ukamkana... Wajanja sehemu kama hizo wanakaa kimya wasijulikane wapo upande gani mfano hai Prof Jay na hata AY hawakuwa upande wa Sugu wala upande wa Clouds.

Mwisho wa siku Sugu ndiye aliempa Prof Jay mchongo wa ubunge na kupata nafasi kugombea jimbo akiwakilisha
Chadema huku mgeni kwenye chama.

Enzi Lady Jaydee ana bifu na Ruge, MwanaFa hadharani ukatumika upande wa Rge huku wajanja wenzako wamekaa kimya na mwisho wa siku wanashirikiana na kupeana michongo.

Juzi harusi ya Prof Jay wadau wa game wote wa kitambo walikuwa kama harusi yao vile full ushirikiano kuanzia Lady Jaydee, Sugu, AY na wengineo kibao wewe wamekutenga.

Unaambiwa ndugu wakigombana chukua jembe ukalime... Leo Sugu na Clouds washkaji sana, MwanaFa aibu uliyoibeba unaificha wapi?

Kesho Clouds na Lady Jaydee watapatana tena utaficha wapi aibu?

Tena mwanaFa wewe umeenda shule ungekuwa sio snitch Sugu angekubeba sana wewe nawe ubadilishe maisha yako kwenye upande wa pili.

Leo hata WCB Wasafi wanakuogopa kufanya kitu na wewe wanajua ni snitch..

Jitahidi ubadilike kaka mkubwa...

Wako mshabiki wako toka enzi za Ingekuwa vipi?
 
Nani alikwambia mwana fa alianza nakinasugu au Ay ??? Mwana fa wimbo wake wakwanza ....
Ingekuwa vipi .sasa hapo nasugu au kina ay kina gk wapi nawapi ??

Sent from my TECNO CX Air using JamiiForums mobile app
 
Sio kila ambacho unakiwaza basi ndivyo kilivyo,wasanii kibao tu hawakuwepo kwenye harusi na ukongwe haukua kigezo cha kuhudhuria pia maana kulikua na vitoto kama Harmo na mjini kila mtu na ratiba zake usidhani ni lazima wote wawepo sehemu fulani sina uhakika kama Nature na Mabaga fresh waliudhuria au nao wametengwa.
 
Tatizo ni FA kutohudhuria sherehe au kuwa na tofauti kama ulivyoeleza??

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Alieleta huu Uzi ni Mshamba sana Tena Mzamani kweli kweli!

Mwana FA Ana Maisha yake na Wengine wana Maisha Yao Acha Umbea

Eti Prof J kapewa Ubunge na Sugu? Hujui uwekezaji Mkubw aluofanya Joseph Mwenyewe
 
unajua maana ya mchongo???

Alieleta huu Uzi ni Mshamba sana Tena Mzamani kweli kweli!

Mwana FA Ana Maisha yake na Wengine wana Maisha Yao Acha Umbea

Eti Prof J kapewa Ubunge na Sugu? Hujui uwekezaji Mkubw aluofanya Joseph Mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…