Kimetah
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 1,049
- 189
Ni rahisi sana kuwa rafiki wa kweli. Jitahidi katika maisha yako kuwa rafiki wa kweli. Jitahidi. Jaribu haya machache;
1. Hupendi anachokipost: Usitukane. Usimkebehi. Usimseme kwa rafiki zake. Usimdharau. MSHAURI. MWAMBIE VILE UNAVYOFIKIRIA.
2. Anaandika kile usichokiamini: usitukane. Usipuuze. JADILIANA nae. MUELIMISHE. Kubali KUTOFAUTIANA kwa hoja.
3. Ana akili na maarifa zaidi yako: Usijenge chuki. Usimchukie kimya kimya. Usiwe na roho ya husda. Usimfitini. JIFUNZE KUTOKA KWAKE. TUMIA MAARIFA YAKE. MTIE MOYO.
4. Umemzidi kwa mambo mengi: Usimdharau. Usimpuuze. Usimtenge. MSAIDIE AFANIKIWE. MSHAURI. MUONYESHE NJIA.
5. Ana tabia usizozipenda. Ni mlevi, malaya, tapeli, muongo, mlaghai, ana wivu, mchochezi, fitna: Usimchukie. MPENDE ZAIDI. MSAIDIE. MSHAURI. MLINDE. MUUOMBEE. MSHAURI TENA.
6. Huwezi kufanya hayo: ACHANA NA MAISHA YAKE. ISHI MAISHA YAKO. Usifuatilie kapost nini, kaandika nini, amevaa nini, ana mpenzi gani, anafanya kazi gani, anaishi wapi, amekula nini nk.
Acha kumfuata Instagram, FaceBook, Twitter, Mtaani nk. Msahau kama yupo. Bado utakuwa rafiki wa kweli.
Ishi maisha chanya kwa kujitahidi kuwa rafiki wa kweli. Kwa kuishi vizuri na watu maisha yako yanakuwa bora zaidi. Usijifikirie mwenyewe. Hauishi kama kisiwa.
Unafiki ni tabia ambayo mwenye nayo hajui. Yeye anaona yuko sawa. Lakini ndani yake moyo wake unauma na roho yake inasagika. Usitake kuishi maisha hayo