Mwana JamiiForums Faizafoxy yupo wapi?

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Jamii forum ni kama familia, tena familia kubwa sana japo hatufahamiani wala kuonana lakini makala zetu na michango yetu humu jukwaani imetufanya tukafahamiana hata kwa itikadi za kisiasa.

Mimi binafsi kuna member nimekuwa nikiwafuatilia kwa muda mrefu sana na kupenda kusoma makala zao, mmoja wapo ni huyu member aitwaye Faizafoxy ambaye sijamuona kwa muda mrefu sana humu jukwaani.

Kama ni buheri wa afya angefanya hata kuja mara moja kusalimia na kutoa hata maoni yake juu ya miradi mikubwa miwili iliyoanza kazi na Kuitetemesha Tanzania na Duniani nzima kwa ujumla, kwa namna mama wa shoka Mama Samia alivyo imaliza kibabe na kihodari.

Miradi hii ni ule wa SGR pamoja na ule wa bwawa la mwalimu Nyerere ambapo mtambo namba Tisa umewashwa ambao unazalisha megawati 235 ambao ni zaidi ya vinu vyote vya bwawa la kidatu linalozalisha megawati 204 na Mtera megawati 80.

Ningemuomba mama huyu Faizafoxy kama anapitia humu aje atoe hata mchango wake juu ya historia ya kipekee kabisa iliyoandikwa katika Taifa letu hili la Tanzania.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Umesahau no za sim mkuu?
 
Kaenda kupigana vita sasa naona kama bomu limepita nae[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Le Mbebez FaizaFoxy unaitwa huku.

Amejitokeza mposaji, labda mwaka huu tutakula basmat la harusi😀
 
Hadi unakosa amani kisa humuoni,
Hadi unajua Faizafoxy hayupo jukwaani,
Unampenda... fanya uwe na namba yake na ya ukoo wake uwe unapiga kumuulizia
Hapana ephen yule ni mama yetu mimi na wewe. Ni kama wewe ukikosekana humu jukwaani lazima nitafahamu haraka sana maana huwa ni lazima nikuangalie kama upo au haupo.japo unaweza usifahamu kama nipo karibu yako kuriko hata kimvuli chako cha mchana.

Unaendeleaje lakini ephen?
 
Kaozeshwa ndoa ya mkeka
 
Ni vema ukafuata Sheria hii sio habari ya Kisiasa at best ni Mahusiano na Mapenzi omba mods waipeleke huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…