Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Ni usiku ambao nimejilaza kitandani natafakari ndugu yangu wewe jinsi ambavyo tumekutana humu JF miaka kadhaa iliyopita. Sikudhani kama ingetokea tukakutana na kuwa washirika wakubwa wenye kujaliana.
Usiku huu napokukumbuka nawaza moyoni je upo mahali salama? Je umeweza kula na kushiba leo? Je umetimiza mipango yako ya leo?
Ni mengi ningeuliza lakini yatosha kusema
usiku huu mwana JamiiForums mwenzangu pumzika kwa amani hapo ulipo.
Mshukuru Mungu hata kwa hicho ulionacho kidogo. Amani iwe nawe na ninasisitiza pumzika kwa amani. Sahau shida zako hata kwa kitambo ili moyo wako nao upate muda wa kupumzika. Usiutese sana kwa mawazo.
Pumzika kwa amani. Mungu alikupenda akakuumba nami nakupenda pia.