Elections 2010 Mwanachama wa CHADEMA (Mkoloni) alishwa sumu Sinza

Elections 2010 Mwanachama wa CHADEMA (Mkoloni) alishwa sumu Sinza

Mutu

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2008
Posts
1,329
Reaction score
49
Mkoloniweb.jpg


Habari za kuvunjika vunjika zilizoifikia JIACHIE mapema leo (jana) asubuhi zinaeleza kuwa mmoja wa Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Fred Marik a.k.a Mkoloni (kulia) ambaye pia ni Mwanachama wa chama cha CHADEMA inadaiwa leo mapema asubuhi akiwa ameambatana na msanii na mwanachama mwenzake G.Solo walikwenda kupata kifungua kinywa maeneo ya MEEDA BAR-Sinza jijini Dar.

Inadaiwa kuwa wote wawili waliamua kupata mtori eneo hilo,lakini katika hali isiyo ya kawaida mmojawao (Mkoloni) akaanza kujisikia vibaya kwa kusumbuliwa na tumbo na kuanza kuishiwa nguvu,Habari zinazidi kudatisha kuwa baada ya kutokewa na hali hiyo ikabidi watu wamkimbize haraka zahati ya karibu maeneo ya Palestina-Sinza kwa huduma ya kwanza.

Source: Food For Thought

Habari zinaeleza kuwa mara baada ya kufika kwenye zahanati hiyo na kuchukuliwa vipimo,ikabainika kuwa bado tatizo halijaonekana kuwa ni nini ama ni kitu gani, hivyo wakashauriwa waende hospitali ya Mwananyamala kwa vipimo zaidi,kukawa hakuna namna ikabidi wampeleke hospitali ya Mwananyamala ambapo mgonjwa huyo alipatiwa vipimo na kubainika kuwa alichokunywa kilikuwa kimewekwa madawa ya kulevya, Kwani mgonjwa huyo alikuwa akikoroma sana na kuonekana kama mtu aliyepoteza fahamu..

UPDATE 2:

Kwa mujibu wa taarifa zilizokuwa zikiingia ndani ya JIACHIE , ni kwamba msanii huyo bado amelazwa katika hospitali hiyo kwa matibabu zaidi.Wadau habari ndiyo hiyo tuendelee kuvuta subra zaidi kwani kuna mdau mkubwa wa JIACHIE amenitonya anakwenda hospitalin

UPDATE 3:

"Ndugu yetu Mkoloni bado hali si shwari sana, hivi anahamishwa kutoka Mwananyamala, kuelekea Muhimbili, sumu imeondoka tatizo limebaki kwenye macho, tuzidishe sala jamani.Si alikuwa hajaamka, kaamka, anaongea kwa taaabu sana,lakini pia anasema macho yanauma na akijitahidi kuangalia hivi, anaona vitu viwili viwili... Kama ukisimama wewe mmoja anawaona wawili,Yah tangu saa tano hivi ndio kahamishiwa huko",

Source wa JIACHIE/Ahmed Michuzi
 
Maoni yangu tutafika kweli namna hii,inatakiwa uchunguzi ufanyike na ibainike nani aliyefanya hivyo.Raha sivyo Tz si mahala salama tena habari zingine za Mwanza mashaka sana .
 
Tumekuwa WAUWAJI sasa? Kisa nini? Ubunge? Urais?

Mwe! Mie simo!

Meeda Bar WATAWAJIBISHWA! Polisi wanatakiwa KUWAKAMATA wahusika wote pale, tena HARAKA, kabla hawajatoroshwa. This is CRIMINAL!
 
Wafanyakazi wa hiyo bar wakamatwe ijewanatumiwa namafisadi wa ccm
 
Dah!Meeda kilikuwa kijiwe hiki enzi zangu za UDSM na life off campus...miaka imeenda.Tukio kama hili ndo litashusha imani za watu kwa kijiwe chenyewe!
 
napata tabu sana kuweka kichwani... hivi kama ni kuua kwa sbabu ya siasa utaanza na mkoloni? au slaa na wagombea wengine?
 
napata tabu sana kuweka kichwani... hivi kama ni kuua kwa sbabu ya siasa utaanza na mkoloni? au slaa na wagombea wengine?
Usipate tabu sana! Labda ana kipindupindu...
 
Kama kawaida ya Chadema wanataka wahurumiwe ndio style yao ya kuomba kura, msishangae mtasikia utumbo mwingi toka chama cha wachungaji!!!!
 
Meeda si ndipo alipigwa risasi mfanyabiashara mmoja na mtu asiyejulikana halafu baada ya miezi kadhaa baadaye mheshimiwa TIBAIGANA alikutwa anatanua na gari la marehemu!!!?
Meeda hii hii.
Kuanzia kesho ntakuwa nakula home kuanzia supu, kitimoto, goulash, bomu, trupa na kadhalika ili kuepuka kutolewa roho mapema na wenye uchungu na nchi hii (hasa uchungu wa madaraka)
 
Mmmh! Meeda? Kesi za namna hiyo zinatokea usiku Kwenye Night clubs mbalimbali... Usijekuta alikesha pale... Akawekewa na CHANGU!
 
inasemekana inawezekana alikuwa anawekewa sugu kwani sugu,gsolo na Mkoloni hicho ni kijiwe chao kikubwa kumbe siku hiyohiyo sugu alisafiri labda waliopewa maelekezo walishindwa kutofautisha sugu na mkoloni na inawezekani sugu sababu ya Chadema ubunge + Antivirus album.
 
Back
Top Bottom