Mwanachuo kuajiriwa na ambae hakufika chuo

Mwanachuo kuajiriwa na ambae hakufika chuo

Joined
Jan 19, 2018
Posts
7
Reaction score
2
Hali imebadilika miaka hii, Wasomi (wanavyuo) wanalalamika ajira kubwa zaidi ni kuwa wanaajiriwa na watu ambao hawasoma elimu ya juu.

Mwanachuo unategemewa na jamii kuanzisha fursa ili uajiri watu.

Mwanachuo wewe ni kioo cha jamii, unategemewa kutoa maamuzi ya busara katika jamii yako katika kutatua changamoto

Mwanachuo usikubali watu wa jamii yako waseme "mhhh wasomi wa siku hizi" ukipita mtaani.

Mwanachuo usiigize maisha, Fanya kazi kwa bidii na kwa akili.tumia kila fursa unayoiona.Usidharau kazi.

Mwanachuo tumia elimu yako, ubunifu wako kutengeneza fursa kwa ambao hawajapata nafasi ya kusoma elimu ya juu (chuo)

Mwanachuo unategemewa na familia yako, jamii yako, Taifa lako kwa ujumla. USIJISAHAU
 
Skuizi hasa makampuni ya wahindi,wachina wamekuwa
Mstari wa mbele kuajiri watu wenye elimubya Diploma kushuka chini ili kuepuka garama na usumbufu mbeleni

Kuna makampuni mengine kama viwanda vya wachina na wahindi wamekuwa wakichukua zaidi vijana wa veta kwa kazi nzito nzito tu ambazo sehem nyingine zinafanywa na watu wenye hadhi ya eng.

Lakini cha kushangaza vijana wa veta wamekuwa wakizipiga hizo kazi tena kwa ustadi mkubwa tu ,lakini wamekuwa wakiminywa kwenye mishahara na ndio kitu mhindi anataka
 
Hali imebadilika miaka hii, Wasomi (wanavyuo) wanalalamika ajira kubwa zaidi ni kuwa wanaajiriwa na watu ambao hawasoma elimu ya juu.

Mwanachuo unategemewa na jamii kuanzisha fursa ili uajiri watu.

Mwanachuo wewe ni kioo cha jamii, unategemewa kutoa maamuzi ya busara katika jamii yako katika kutatua changamoto

Mwanachuo usikubali watu wa jamii yako waseme "mhhh wasomi wa siku hizi" ukipita mtaani.

Mwanachuo usiigize maisha, Fanya kazi kwa bidii na kwa akili.tumia kila fursa unayoiona.Usidharau kazi.

Mwanachuo tumia elimu yako, ubunifu wako kutengeneza fursa kwa ambao hawajapata nafasi ya kusoma elimu ya juu (chuo)

Mwanachuo unategemewa na familia yako, jamii yako, Taifa lako kwa ujumla. USIJISAHAU
Easy said than done
 
Hii inakaaje mkuu?
Wamiliki wa vitengo vya biashara na huduma wasio na elimu ya juu waajiri watu wasio na elimu?!!!!!!!!!!!!!!!&&$&%@#)*?

Kila mtaalam afungue shughuli yake ya uchumi? Afanye kazi peke yake kwa kuwa hakuna mtaalamu wa kuajiriwa?? Uhalisia uko vipi?

Waajiriwa wengi wenye malalamiko, na hata hupelekea kuacha ama kuhama hama kazi mara nyingi ni kutokana na uongozi mahala pa kazi. Hiyo ndiyo inahitji kujadiliwa na kuwapa ukweli waajiri na wasimamizi wa kazi kwa kuwa uongozi mbaya unaharibu kila kitu. Na uongozi mbaya upo katika kila sehemu kwenye private sector, lakini zaidi sana public sector.

Wafanya kazi wanafanya kazi kama wako kuzimu kwa ajili ya uongozi mbovu ambalo ni tatizo kubwa hapa kwetu na kwingineko.
 
Tuache unafiki hapa tunalaumu graduate badala ya kuangalia chanzo nini! Ukweli ni kwamba vyuo hapa Tanzania vinatoa kozi ambazo hazihitajiki mitaani au kozi ambazo zinaenda na dunia ya sasa. So mtu unatoka chuo ukija mtaani hakuna kazi. Ukiangalia kuna maelfu ya ajira mpya zinatengenezwa duniani kila siku lakini sisi tunaendelea kufundisha kozi ambazo hazina soko na kitu kibaya zaidi tunakosa uongozi wa kuchagua kozi ya kusoma vyuo vikuu ukitaka kuamini angalia thread za watu wanaomba ushauri wa kozi za kusoma chuo kikuu.
 
yote maisha kijana.... bill gates hakuwa flesha san dalasani ila leo kaajili vichwa vilivokuwa vinamkimbiza..... alaf wengne hawajasoma ila walizaliwa wakikuta wameshaandaliwa maisha so kuajiliwa nao ni kitu cha kawaida... pia kumbuka tofaut ya dalasa la 7 na chuo mwaka wa tatu ambapo wengi humaliza chuo kuna miaka 9 so wakat ww unasoma hii miaka 9 yeye alikuwa uraian akitafuta so kama aliitumia vema bhas wakat ww ni ndo unahitimu yeye tayari ni boss
 
Wewe na degree yako cha kuanagalia ni mshahara unao lipwa tu, usijali unalipwa na nani. Wewe umesoma miaka yote hiyo 9 ili u qualify kulipwa laki sita kwa mwezi na mwenzako alipambana ili baada ya miaka 9 aingize milioni 60 kwa mwezi, hapo kila mtu amevuna alicho panda. Kama umepata ulicho tafuta tatizo nini?. Kama vipi endelea mapaka PhD ili ukalipwe milioni tano kwa mwezi na hishima kibao ofisini wakati mwezako wa la 7 ameshaongeza makampuni na anaingiza mil 200 kwa mwezi. ZINGATIA kijana " Maisha yanaanza baada ya chuo" huko chuoni ulikua inajiandaa tu na usihangae hata hayo uliyo jiandaa nayo usiyakute huku mtaani tuna somo tofauti.Chuoni mnaanza na lecture kisha mtihani ila Huku kitaa unaanza na mtihani kisha lecture inafuata kusahihisha makosa. SAWASAWA?
 
Back
Top Bottom