Mwanadamu yeyote ana tabia ya kujisahihisha, kujirekebisha, na kubadilika.

Mwanadamu yeyote ana tabia ya kujisahihisha, kujirekebisha, na kubadilika.

Dr Salla

Member
Joined
Aug 22, 2013
Posts
16
Reaction score
22
Nimesema maneno hayo yaliyopo kwenye kichwa cha habari ya makala hii kutokana na namna ambavyo watu wengi walivyojitokeza kukosoa uteuzi wa Profesa Mchome kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Mimi ni kati ya watu wa karibu kabisa ambao tumewahi kufanya kazi na Profesa Mchome kabla hajateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Kimsingi yote yamesemwa lakini sijasikia watu wakimsemea kwa mazuri aliyoyafanya. Sasa ngoja niyataje mazuri machache ya Profesa huyu aliyoyafanya wakati akiwa Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Vyuo Vikuu hapa Nchini.

1. Alileta kitu kinachoitwa 'Minimal Standards for Admission into the Higher Learning Institutions'
Mliomaliza kidato cha sita kuanzia Mwaka 2010 mpaka mtakumbuka kuwa kwa elimu ya Chuo Kikuu mtu akiwa na alama za ufaulu 4.5 katika mchepuo wake anaweza kudahiliwa katika elimu ya Chuo Kikuu. Kutokana na hili wanafunzi wengi wameweza kupata fursa ya kuingia chuo kikuu lakini hapa watu wanazungumzia habari za wanafunzi waliodahiliwa kisha wakashindwa kupata mkopo ila ikumbukwe kwamba Profesa huyu alikuwa hashughuliki na mikopo bali alikuwa anashughulikia masuala ya elimu ya juu kwa kiwango cha udahili, usajili wa vyuo, ubora wa elimu na mengineyo yanayofanana na hayo. Kwa upande wa shahada ya uzamili siku hizi mtu akiwa na G.PA ya 2.7 anaweza kudahiliwa kwenye chuo chochote kwa ajili ya kusoma shahada ya uzamili. Suala la mtu kuomba mkopo wa kusoma chuo kikuu ni hiari na wapo watu ambao huomba kudahiliwa na wamedahiliwa kusoma elimu ya juu lakini hawadhaminiwi na bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.


2. Alileta kitu kinachoitwa 'Central Admission System' tunafahamu kwamba mtu akimaliza kidato cha sita alikuwa anajaza fomu za vyuo vyote alivyotaka kusoma programu anayoitaka halafu mwisho wa siku akipata hata vyuo vyote basi anachakua chuo kimoja anachokipenda jambo ambalo liliwafanya watu wengi kukosa nafasi za kusoma Chuo Kikuu lakini huyu Profesa alileta CAS ambayo unalipa ada ya kudahiliwa mara moja tu na unapata chuo. Sasa kama mtu anajaza fomu kwa makosa je ni suala la kumlaumu huyu Profesa? mambo mengine inabidi tubadilike jamani maana hata ulimwengu unabadilika sana kutoka analojia kwenda digitali.Pia Changamoto au udhaifu wowote ule katika taasisi yoyote ile ni jambo la kawaida embu tukumbuke ukiritimba wa UDSM, Mzumbe na vyuo vingine ambao ulikuwepo katika mchakato wa kudahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo kikuu kabla ya Mwaka 2010? Je mara hii tumeshasahau mtihani wa matriculation?

3. Kusimamia ubora wa Mitaala ya elimu vyuoni ni moja ya kazi alizoanza kufanya Profesa huyu ambapo mitaala mbalimbali ya vyuo vikuu hapa nchini imekuwa ikipitiwa mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa ina ubora.

4. Alileta kitu kinachafahamika kama Credit Accumulation Transfer ambapo kwa sasa kama mtu ana dharura ama tatizo kubwa kabisa linalomzuia yeye kusoma kwenye chuo husika au kwa sababu nyingine yoyote basi mtu huyo anaruhusiwa kuhama kutoka chuo kimoja kwenda kingine.

5. Amepiga marufuku sana uanzishwaji wa Vyuo feki na ujenzi wa vyuo holela usiofuata utaratibu. Kwa mfano Chuo Kikuu Cha TEKU kiliwahi kujenga kampasi Dar es Salaam na kuanza kufundisha bila ya usajili na profesa akaifunga kampasi hiyo na nyingine nyingi ambazo zilikuwa feki. Zote zilifungiwa na watuhumiwa walifikishwa mbele ya sheria.

Kwa leo nimeanza na hayo japo kuwa Profesa Mchome ni binadamu na siyo malaika kwa hiyo kuna kukosea lakini tufahamu wazi kabisa kwamba mabadiliko siyo tukio bali ni mchakato. Wakati mwingine pamoja na ukosoaji ambao unaweza kuibuka kutokana na makala hii lakini hata pale mtu anapofanya jambo zuri basi tuheshimu na kupongeza jitihada zake jamani!
 
Back
Top Bottom