Uchaguzi 2020 Mwanadiplomasia Goodluck Ng'ingo, achukua fomu na kurudisha ya kugombea Ubunge jimbo la Kalenga

Uchaguzi 2020 Mwanadiplomasia Goodluck Ng'ingo, achukua fomu na kurudisha ya kugombea Ubunge jimbo la Kalenga

sweetlee

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2015
Posts
4,050
Reaction score
14,770
Kuelekea Uchaguzi Mkuu October,Siku ya jana tarehe 16/7/2020 Mwana Diplomasia na Mchambuzi wa masuala ya Siasa Goodluck Ng'ingo alichukua fomu na kurudisha ili aweze kupata ridhaa ya kugombea Ubunge Kalenga.

Kufuatia mazungumzo yake mengi na vyombo mbalimbali vya Habari vya ndani na nje ya nchi amekuwa akisisitiza sana viongozi kuwa daraja kati ya wananchi na serikali yao.

Aliwahi kusema "Majukumu ya Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwa kiungo kati ya wananchi na Serikali Kuu, kuwa kichocheo kikubwa cha shughuli za maendeleo kwenye Jimbo".

Akiendelea kusisitiza kuwa "Mbunge anatakiwa ahakikishe sheria zinazotungwa zinaakisi uhalisia na mahitaji ya mwananchi, kwahiyo mwananchi kama kuna sheria inambana ajue kwamba kuna Mbunge alishindwa kumwakilisha vyema Bungeni"

Haitoshi tu kusema anajua majukumu ya mbunge, majukumu yake kama kiongozi wa wananchi lakini anatosha kuwa kiongozi hasa wa wana Kalenga.

Kila la kheri kwako Mungu akutangulie.

IMG-20200716-WA0028.jpg
IMG-20200716-WA0026.jpg
IMG-20200716-WA0027.jpg
IMG-20200716-WA0023.jpg
 
Ng'ingo kikwetu ni ngozi! Kila la heri mwagito
 
Mliambiwa na Polepole kuwa kampeni haijaanza, hivyo, ni kosa kuanza kufanya kambeni kwa kutumia mitandao ya kijamii
 
Mliambiwa na Polepole kuwa kampeni haijaanza, hivyo, ni kosa kuanza kufanya kambeni kwa kutumia mitandao ya kijamii
Nioneshe nilipopiga kampeni? Hizo ni pongezi zangu kwake sijakuambia umchague. Relax kunywa maji mengi utoe makasiriko.
 
Bora amtoe yule teja Milinga. Maana kwa muda alio kaa bungeni michango yake ilikuwa ya kipumbavu tuu. Sijui ana elimu gani yule mtoto. Na kama amesoma ni labda sanaa ya kiganga
 
Bora amtoe yule teja Milinga. Maana kwa muda alio kaa bungeni michango yake ilikuwa ya kipumbavu tuu. Sijui ana elimu gani yule mtoto. Na kama amesoma ni labda sanaa ya kiganga
Jamaa kalala sana hakuna alichofanya bungeni.
 
Back
Top Bottom