Kwani wasanii wa Bongo Fleva beats wanatoa wapi? Tanzania hatuna muziki wa Zouk, Kwaito, Reggae, bali ni rumba iliyotoka Congo/Kinshasa na wao wali imodernize kwani asili ya huu muziki wa Congo ni Cuba na ulikuwa unaitwa Afro - Cuban. Tanzania na Congo in the 1950's (late) tukaja na style yetu ya kiafrika na kuachana na ile ya Cuba (salsa/charanga). Hivyo muziki wa asili wa tanzania ni rumba dizaini ya msondo na Sikinde, ila hii ya Bongo Fleva si miziki yetu lakini utashangaa mtu hapa Tanzania anaitwa malkia wa Zouk, au mfalme wa Kwaito, sasa wenye huo muziki waitwe nani, wababaishaji? Hakuna msanii wa Fleva hapa Bongo mwenye beats zake, wote hawa feki wanakopi tu. Diamond kwa sasa anatumia beats za Nigeria, Jay Dee Kwaito, yaani mambo ya kukopi tu na ku paste, inaboa kishenzi. Dully lazima akasirike kwani kakamatwa na hakutegemea kama kuna watu wanajua ile beats. Masuala ya ushoga kwani yeye pia si kuna jamaa walimtwanga kisamvu chake/kumshikisha ukuta miaka ya nyuma baada ya kulala na mke wa mtu? Sasa yeye aitwe nani?