Mwanafalsafa anamkaribisha nani 'asanteni kwa kuja'? Kweli huyu ni Mwanafalsafa

Mwanafalsafa anamkaribisha nani 'asanteni kwa kuja'? Kweli huyu ni Mwanafalsafa

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
4,664
Reaction score
9,929
Habari zenu wadau wa burudani,

Mwana Falsafa katoa wimbo mpya, jina "Asanteni kwa kuja". Ukisikiliza kwa haraka haraka ni ngumu kaelewa kaimba nini ana maana gani;

Je, anamwimbia mwanamke? Hapana.
Je, anasifia anasa? Hapana.
Nini sasa anaimba?

Kujua anachoimba sikiliza ubeti wa pili na wa tatu. Kwakuwa muziki ni sehemu ya fasihi, basi kila mtu anaweza pata maana yake ila dhamira ya mtunzi huwa haitofautiani sana hata kama kila mchambuzi atakuja na maana nyingi nyingi.

Nini sasa nilichoona? Samahani sitaji uchonganishi ila hii ndio nilichoona;

Mwana falsafa anawambia wasanii waliomkuta katika game na wamepata mafanikio ila sasa wanaleta dharau kisa wana pesa ila hizo pesa haamini kama wanazipata kutokana na mziki kwani yeye anaujua huu mziki.

Wasanii wepi? Au nani? Miye na wewe hatujui!

Sikia anakwambia, "Tatizo la uwongo haufiki mwisho utatudanganya utaacha kiporo..". Sikia anasema, "IIlikuwa pouwa tu kabla mkwanja haujaleta makuu.."

Pamoja na yote anawashukuru hawa wasanii waliomkuta katika game kwani wameleta changa moto. Naomba nishie hapa, ukipata mda utafute huu wimbo usikilize.
 
Hawa jamaa Diamond atawaburuza sana.
 
Mwana F A mi namkubali sana, ila achunge kauli zake.
 
Msitake kuchonganisha jamaa angekuwa na wivu angeoneka kwenye Video za wasanii wengine? Ni kazi ya Sanaa tu. Kila mtu anauelewa ujumbe kivyake kwahiyo msitake kulazimisha paranoia zenu ziwe ukweli. Hakuna majungu hapo
 
Wewe utandu huo wimbo alioponda hao watu ni UPI?
Au una version 2?
 
huyu nae mkubwa mzima kwenye game kitambo lakini anashabikia kijani kama madogo kina diamond... ndio maana haendeleiiii..

levo zake ni kina sugu, prof jay, Ay na wengineo... ila yeye mkubwa mzima anapanda majukwaani kuwasifia kijani kama watoto kina diamond
 
duh, kwahiyo ccm ni ya watoto
 
huyu nae mkubwa mzima kwenye game kitambo lakini anashabikia kijani kama madogo kina diamond... ndio maana haendeleiiii..

levo zake ni kina sugu, prof jay, Ay na wengineo... ila yeye mkubwa mzima anapanda majukwaani kuwasifia kijani kama watoto kina diamond
Maisha yake ni movie, na yeye ndo director.

Hata ukimuelekeza basi itakua ni extra
 
huyu naye anapendaga swaga za jigga..mzee wa copy and paste...wimbo izzo wa jigga anafungua na maneno haya"thank you for comin,you coulda been anywhere in the world but here with me"
 
Wakiitwa mashabiki wa Hamisi nitakua kati ya wale wa mwanzo kabisa ila hii ngoma hajatenda haki kwangu imekua nyepesi sana ingawa nimejitahidi kuisikiliza mara nyingi sana na sijaona sababu ya kua kimya kwake kama amerudi ivi,umri unaondoka na uandishi wake unamuacha na style yake.
Thanks for coming......!
 
Namuelewa!!!
Thanks for coming Hamis, and u can stay kabisa!!!
 
kwa sababbu ni ccm i dont care.mi nasikiliza nyimbo za sugu,af sele,na prof j
 
Mie hata sijausikia,ngoja nitautafuta.
 
Back
Top Bottom