REJESHO HURU
JF-Expert Member
- Mar 6, 2014
- 4,664
- 9,929
Habari zenu wadau wa burudani,
Mwana Falsafa katoa wimbo mpya, jina "Asanteni kwa kuja". Ukisikiliza kwa haraka haraka ni ngumu kaelewa kaimba nini ana maana gani;
Je, anamwimbia mwanamke? Hapana.
Je, anasifia anasa? Hapana.
Nini sasa anaimba?
Kujua anachoimba sikiliza ubeti wa pili na wa tatu. Kwakuwa muziki ni sehemu ya fasihi, basi kila mtu anaweza pata maana yake ila dhamira ya mtunzi huwa haitofautiani sana hata kama kila mchambuzi atakuja na maana nyingi nyingi.
Nini sasa nilichoona? Samahani sitaji uchonganishi ila hii ndio nilichoona;
Mwana falsafa anawambia wasanii waliomkuta katika game na wamepata mafanikio ila sasa wanaleta dharau kisa wana pesa ila hizo pesa haamini kama wanazipata kutokana na mziki kwani yeye anaujua huu mziki.
Wasanii wepi? Au nani? Miye na wewe hatujui!
Sikia anakwambia, "Tatizo la uwongo haufiki mwisho utatudanganya utaacha kiporo..". Sikia anasema, "IIlikuwa pouwa tu kabla mkwanja haujaleta makuu.."
Pamoja na yote anawashukuru hawa wasanii waliomkuta katika game kwani wameleta changa moto. Naomba nishie hapa, ukipata mda utafute huu wimbo usikilize.