SoC02 Mwanafamilia mpya

SoC02 Mwanafamilia mpya

Stories of Change - 2022 Competition

Anna Meleiya Mbise

New Member
Joined
Sep 7, 2022
Posts
3
Reaction score
0
Jina la Shairi: Mwanafamilia Mpya

Jina la Mwandishi: Anna Meleiya Mbise


1.Wanaita digitali, zama zimebadilika,
Na wala si ajali, ndio pilikapilika,
Twazipata kihalali, kutunza tunachemka,
Simu wewe ndio nani, mbona unatunyoosha?

2.Mimi niliponunua, kwanza nilijiuliza,
Hii simu yala mua, au mchele na panza,
Sisi miwa twakamua, simu vocha unajaza,
Nani aliemjanja, asolisha digitali?

3.Wakati nikikulisha, rohoni nasema sio,
Japo unaniamsha, wako mororo mlio,
Mawazo nayahamisha, kukiepuka kilio,
Simu inaweza kula, na mimi nishinde njaa.

4.Asante nyingi za Voda, na za Tigo utalewa,
Kulongalonga washinda, siku nzima wanogewa,
Wapoteza wako muda, ukilonga na Kidawa,
Wandungu nambieni, ni raha ama karaha.

6.Na biashara haramu, yakuunza mahekalu,
Asha Ida Mariamu, anawachuma Masalu,
Yawaleta kwa awamu, kupanga ilifaulu,
Epuka kuparamia, jitambue imiliki.

7. Tumezipa na jukumu, kwa vile tunazilisha,
Kulea twazipa zamu, na pia kutuamsha,
Kwao si kazi ngumu, watoto kuburudisha,
Chonde tuweni makini, huyu ni ndugu wa kambo.

8. Uongo ulo kithiri, simu zinakaribisha,
Yupo karibu akiri, kumbe kaenda Arusha,
Mikopo ni utitiri, M-pawa na songesha,
Simu haina ajizi, inakula kama mchwa.

9. Zinajua mengi simu, na hamna pingamizi,
Wengi mtakunywa sumu, zikiamua uwazi,
Tumezifanya muhimu, wa siri zetu mlinzi,
Ndugu huyu machachari, kashatuzidi akili.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom