Mimi sio mwalimu lakin ningekuwa mwalimu zaidi ningependelea adhabu ya assignment kwa mtoto , mpe mtoto topic apresent hata wiki mbili mfululizo hii itamuweka bize na kumuongezea uelewa.Walimu achaneni na adhabu za hovyo
Namkumbuka Mwalimu wetu wa Biology
Alitupa adhabu ya assignment,,mwanzo mwisho topic zote
Jumla ya maswali kama 500 hivi.
Biology ilikuwa inaniboa
Lakini hayo maswali yalisaidia sana hadi necta.
Ilikuwa ni lazima kusoma somo lake,na anataka kuona summary ya ulichosoma
Akaweka utaratibu wa kukagua mara 2 kwa wiki
J3 anakagua ulichosoma weekend
Ijumaa anakagua ulichosoma j3 Hadi alhamisi..
Na anataka hizo summary uweke kwenye file.
Akija kukagua ni anakuuliza maswali,kwahiyo siyo suala la kucopy tu notes km summary
Hapo ukikosa ni fimbo.
Mtu anaona kulikoni nitandikwe fimbo kwa kutokusoma
Heri nimeze..
Huandiki summary kama pambo,bali unaandika ulichokisoma na kukiweka kichwani.
Huna summary hapo ni fimbo tena.
Walimu wangechukua hii mbinu kwa kiasi ingesaidia watoto.