Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Na SHABAN MAKOKHA
SHEREHE za kutuza mshindi wa kula boflo na kunywa soda jana ziliishia simanzi, baada ya mwanafunzi mmoja kunyongwa na mlo huo hadi kufa kwenye Shule ya msingi ya Sikura, Kaunti ya Busia.
Marehemu Harrison Oduor Ouma, alikuwa kati ya wanafunzi waliojawa na furaha akitumai kuwa angeshinda na kutuzwa ila chakula hicho kiilishia kukwama kooni na kwa masikitiko makubwa, kusababisha mauti yake.Shindano hilo liliidhinishwa na usimamizi wa shule hiyo.
Juhudi za walimu na wanafunzi wenzake kumpa huduma za kwanza hazikufanikiwa kwa kuwa alifariki akikimbizwa hospitalini.“Alinyongwa na kipande cha mkate ambacho kilikwama kwenye koo lake kisha akapoteza famu licha ya kupokezwa huduma ya kwanza na walimu pamoja na wanafunzi wenzake.
“Usimamizi wa shule hiyo ulihakikisha kuwa anakimbizwa hospitalini lakini kwa masikitiko makubwa, akafa kabla ya kufika katika zahanati ya Buluani, mita chache kutoka shule hiyo,” akasema Mkuu wa Polisi wa Kaunti ndogo ya Butula, Bw Jacob Chelimo.
Wanafunzi walikuwa wakishiriki mashindano hayo ya kula mkate na kunywa soda siku ya mwisho wa muhula huu kabla ya kuenda likizo ya sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya.Bw Chelimo alithibitisha kuwa Mwalimu Mkuu, Bw Peter Tetela alipiga simu na kumwaarifu kuwa mvulana huyo alinyongwa na mkate huo hadi akafa shuleni humo.
Mtaalamu wa masuala ya kimatibabu Dkt Donald Musi amezishauri shule kuepuka tabia ya kuwaruhusu wanafunzi kushiriki mashindano ya kula chakula hasa mikate akisema ni hatari na yanaweza kusababisha vifo.Ingawa hivyo, amependekeza kuwa iwapo lazima mashindano hayo yawe, basi vyakula ambavyo ni vyepesi na haviwezi kumyonga mtu vitumike.
Mwili wake umehifadhiwa katika mochari ya Sega.
Taifaleo