Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Mwanafunzi wa Darasa la sita katika Shule ya Msingi Manzese, jijini Dar es alaam, Ally Omary leo mchana aliopolewa na wasamaria baada ya kuzama kwenye bwawa la maji lenye kina kirefu lililopo karibu na viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilichopo Mlimani. Katika zoezi hilo Kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto cha Halmashauri ya Jiji kilijaribu kuutafuta mwili wa mtoto huyo bila mafanikio mpaka walipotokea wasamaria wanaojua kuogelea na kuamua kupiga mbizi kuutafuta mwili huo.
Chanzo: MWANAFUNZI AFIA MAJINI - Global Publishers
hivi ni kweli hicho Kikosi cha Zima moto kinafanya kazi yake barabara? Wameshindwa kumtowa Mtoto marehemu ndani ya Dimbwi la maji? Ehhhh ndugu zanguni hatuna Serikali jamani tuna Utawala wa nguvu jamani. Poleni ndugu jamaa wa Marehemu mfiwa Mwenyeezi Mungu amuweke pema peponi Marehemu ameen.
Umati ukitafakari jinsi ya kuusaka mwili wa mwanafunzi huyo.
Kikosi cha uokoaji kikingia kazini.
Waokoaji wa kikosi cha Halimashauri ya Jiji wakitumia miti kuusaka mwili wa marehemu lakini waliambulia patupu na kunusurika kupigwa na wananchi wenye hasira.
Ulinzi uliimarishwa eneo la tukio kuwadhibiti wananchi wenye hasira waliotaka kutoa kipigo kwa waokoaji hao baada ya kuwaona huduma zao si lolote.
Wakati zoezi la utafutaji mwili likiendelea ulionekana mwili wa kukualiyechinjwa ukielea kwenye bwawa hilo.
Mwili ukiendelea kutafutwa.
Baada ya kuonekana huduma za waokoaji hao ni za ubabaishaji wasamaria hawa walijitosa kwenye bwawa hilo na kufanikiwa kuupoa mwili wa marehemu.
Wasamaria wakiwa na mwili wa marehemu baada ya kuupoa Kikosi cha Halmashauri kilipochemka.
Kikosi cha Halmashauri ya kikiondoka eneo la tukio.