Mwanafunzi afia majini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Mwanafunzi wa Darasa la sita katika Shule ya Msingi Manzese, jijini Dar es alaam, Ally Omary leo mchana aliopolewa na wasamaria baada ya kuzama kwenye bwawa la maji lenye kina kirefu lililopo karibu na viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilichopo Mlimani. Katika zoezi hilo Kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto cha Halmashauri ya Jiji kilijaribu kuutafuta mwili wa mtoto huyo bila mafanikio mpaka walipotokea wasamaria wanaojua kuogelea na kuamua kupiga mbizi kuutafuta mwili huo.

Umati ukitafakari jinsi ya kuusaka mwili wa mwanafunzi huyo.

Kikosi cha uokoaji kikingia kazini.

[
Waokoaji wa kikosi cha Halimashauri ya Jiji wakitumia miti kuusaka mwili wa marehemu lakini waliambulia patupu na kunusurika kupigwa na wananchi wenye hasira.

Ulinzi uliimarishwa eneo la tukio kuwadhibiti wananchi wenye hasira waliotaka kutoa kipigo kwa waokoaji hao baada ya kuwaona huduma zao si lolote.

Wakati zoezi la utafutaji mwili likiendelea ulionekana mwili wa kukualiyechinjwa ukielea kwenye bwawa hilo.



Mwili ukiendelea kutafutwa.

Baada ya kuonekana huduma za waokoaji hao ni za ubabaishaji wasamaria hawa walijitosa kwenye bwawa hilo na kufanikiwa kuupoa mwili wa marehemu.

Mmoja kati ya wasamaria waliojitolea kuusaka mwili huo akiwa kazini.

Wasamaria wakiwa na mwili wa marehemu baada ya kuupoa Kikosi cha Halmashauri kilipochemka.

Mwili wa Marehemu.


Kikosi cha Halmashauri ya kikiondoka eneo la tukio.

Chanzo: MWANAFUNZI AFIA MAJINI - Global Publishers

hivi ni kweli hicho Kikosi cha Zima moto kinafanya kazi yake barabara? Wameshindwa kumtowa Mtoto marehemu ndani ya Dimbwi la maji? Ehhhh ndugu zanguni hatuna Serikali jamani tuna Utawala wa nguvu jamani. Poleni ndugu jamaa wa Marehemu mfiwa Mwenyeezi Mungu amuweke pema peponi Marehemu ameen.
 
Jamani, mtoto MMOJA tu kadondoka kwenye BWAWA kikosi cha uokoaji kinashindwa kumtoa, vipi ikitokea so kubwa? (Mungu apishe mbali). Niliwacheki jana wanamkacha mtangazaji asiwahoji, wakati anawauliza zoezi limeendaje wanasema limeenda vizuri! Shame on them!!
 
Pumbavu kabisa halafu kodi zetu zinawaendea kwakweli hili linchi letu mwe saa zengine unaweza kumzaba mtu vibao kabisa!!!
 
pumbavu kabisa halafu kodi zetu zinawaendea kwakweli hili linchi letu mwe saa zengine unaweza kumzaba mtu vibao kabisa!!!

inasikitisha sana. Mpka lini hali hii itaendelea nchini petu?!.kwa nn mamlaka zinazofanya uzembe kma huu wa kushindwa kuzingatia sheria za afya na usalama wa watu (health & safety) haziwajibishwi?. Tumepoteza wenzetu wengi kwa uzembe wa hata wa kushindwa kuweka onyo,kuweka mlinzi wa kuchunga sehemu za madhala kma hizi nk...
 
KWANI HAPO WEYE KAZI YAO WANAOGOPA MAJI MPAKA WANATUMIA HIYO MITI,NAONA HAO WATALAMU WAO WANATOKA KWEYE MAWE,
kAZI IPO WANA JF KAMA MASAADA HAUWEZEKANI BASI SIO KUTUZINGUA
cONQUEST-HAKUNA MSAADA MPAKA TUKALIE KITI KAMA KUFA KUFENI SIE NI UCHAGUZI TUU,TUPO KIUCHAGUZI TUU.
 
Sidhani kama wanayafahamu vizuri majukumu yao. Kama wanayafahamu basi they are incompetent
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…