Mwanafunzi aliyeonewa kwa kutoa majibu sahihi.

Mwanafunzi aliyeonewa kwa kutoa majibu sahihi.

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,313
Reaction score
12,170
Mwanafunzi huyu alipata sifuri licha ya kwamba majibu yake yote yalikuwa sahihi kwahiyo usilazimishe kila mtu aamini unachokiamini inawezekana yupo sahihi.


SWALI: Mkwawa alikufa katika vita gani?.
JIBU: Katika vita yake ya mwisho.

SWALI: Mkataba wa Geneva ulisainiwa wapi?.
JIBU: Mwisho wa karatasi

SWALI: Nini sababu kuu ya talaka?
JIBU: Ndoa

SWALI: Kitu gani ambacho huwezi kula wakati wa mlo wa asubuhi?
JIBU: Chakula cha mchana na cha usiku

SWALI: Kipi kinachofanana na kipande cha tunda?
JIBU: Kipande cha pili cha tunda hilo.

SWALI: Hitler alikufa vipi?
JIBU: Moyo wake uliposimama baada ya kufika malaika wa kifo.

SWALI: Vita vya pili vya dunia vilimalizika lini
JIBU: askari walipochoka kupigana.

Tusilazimishane uelewa wa mambo🙂😎😎[/b]
 
Back
Top Bottom