Mwanafunzi ameunda emojis 350 kubadili picha ya umasikini wa Kiafrika

Mwanafunzi ameunda emojis 350 kubadili picha ya umasikini wa Kiafrika

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
O'Plerou Denis Grebet (22), msanii wa Ivory Coast, anaifanya Afrika kujivunia kwa kuweka picha chanya juu ya bara la Afrika ameunda emojis 350 ambazo zinaonyesha uzuri wa utamaduni wa Kiafrika katika aina zote.

Alivutiwa kuunda emojis kuhusu Afrika kwa sababu picha alizoziona kuhusu bara hilo zilimkera. Anapenda sana kuonyesha Afrika katika hali nzuri. Hii imesababisha kuundwa kwa emojis 350 ambazo zinaonyesha uzuri wa utamaduni wa Kiafrika katika aina zote

"Niligundua kuwa vyombo vya habari na Makala nyingi kuhusu Afrika zilikuwa zinazungumza juu ya upande mbaya wa bara pekee. Walifanya picha ya Afrika kuwa nchi ya vita ambayo watu ni maskini na wenye njaa. Vitu hivi ni kweli lakini havipo kila mahali kwenye barani afrika ," alisema.

Ukurasa wake wa Instagram umejazwa na picha nzuri zinazoonyesha aina tofauti za sanaa za tamaduni za Kiafrika

"Haikuwa ngumu sana kwa sababu najua jinsi ya kuchora kwa mkono wangu, kwa hivyo, ni kama mimi tu nimehamisha ujuzi kwenye kompyuta," alisema

Vipande vina ubunifu mwingi na vimempa umaarufu sio tu kwa wanafunzi wenzake, bali pia kati ya wananchi. Sanaa yake ni ishara kwamba Afrika ina vitu vikubwa ya kusema na inashikilia uzuri ambao unaweza kustaajabisha ulimwengu wote

2020-01-16 (2).png
2020-01-16 (3).png
2020-01-16 (4).png
 
Pale jamaa anayekula ugali inamaa amenyoa ni staili pya au ndo kusma anaumri unaofanana na yeye kama alivyo
 
Safi sana aisee, embu tuwekeeni hizo zingine tuzione bc, ikiwezekana ziingizwe kwenye android kbs
 
Back
Top Bottom