A
Anonymous
Guest
MWANAFUNZI ALIYEPATA AJALI UWANJA WA TAIFA ATELEKEZWA BILA MSAADA WA UVCCM ..!
Mwanafunzi Emmanuel Jackson Malima mwenye umri wa miaka 17 anayesoma kidato cha nne (Form IV) Shule ya sekondari ya Kipunguni alisukumwa na kuanguka akiwa Jukwaani uwanja wa Benjamini Mkapa hata kupelekea kuumia vibaya sana sehemu za kichwa.
Mzazi wa Emmanuel Jackson Malima anasema Mtoto aliporudishwa nyumbani na wenzie walimpeleka ktk hospitali ya Rugambwa Ukonga baada ya kuona karudi na majereha huku akilia kwa uchungu.
Hospitali ya Rugambwa wakasema hawana uwezo na tatizo hilo, ikabidi wampeleke ITEC hospital hapo Upanga,
ITEC wamesema wanahitaji kumfanyia vipimo wa CT scan kichwani na shingoni.
Mwanafumzi Emmanuel Jackson Malima kwa sasa hawezi kula na muda wote analia pamoja na kulalamika maumivu makali anayopata kutoka sehemu ya kichwa na shingoni.
Siku ya tarehe ya 7/7/2024 katika tamasha lililoandaliwa na UVCCM uwanja wa Benjamin Mkapa walijaza wanafunzi kutoka shule zote za Sekondari mkoa wa Dar es saalam kwa kile walichokiita kampeni maalum kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na ushiriki wa vijana katika uchaguzi.
Mzazi wa Emmanuel Jackson Malima amesikitika kwakuwa Mtoto alimuaga anaenda shuleni, ambapo walimu waliwaambia wanafunzi kuwa shule imeandaa magari kwenda uwanja wa Taifa bila kusema kuna shughuli gani.
Hata wao wazazi wa wanafunzi walioenda uwanja wa Taifa hawakujulishwa na Walimu kama kuwa watoto wanaenda ktk shughuli za siasa za CCM huko uwanja wa Taifa.
Emmanuel Jackson Malima mwaka huu anatarajia kufanya mitihani yake ya kidato cha nne, amesukumwa na kuumia vibaya sana
Lakini cha ajabu siyo shule wala UVCCM waliojitokeza kumsaidia au hata kumrudisha nyumbani mtoto wa watu aliyepata ajali katika shughuli yao au kumpa matibabu ya awali.
Wazazi wake Emmanuel ni Wajasilia mali wadogo, wanalazimika kumtibia mtoto wao peke yao bila msaada wa watu waliomchukua mtoto wao katika shughuli za kisiasa bila ridhaa yao.
Na sasa gharama ya matibabu imakuwa kubwa, wanashindwa kuimudu na kuhitaji Watanzania wamsaidie mtoto wao Emmanuel Jackson Malima atibiwe haraka kabla tatizo halijawa kubwa.
Nilipojaribu Kumtafuta Mohammed Ali Kawaida Mwenyekiti wa UVCCM na katibu wake Jokate Mwegelo kutaka kuwauliza kwanini wanakuchukua watoto wa watu mashuleni bila ridhaa za wazazi na baadae kuwatelekeza baada ya watoto kupata matatizo Simu zao zimeita tuuuuuuuuuu bila kupokelewa.
Nimejaribu pia kumpigia msajili wa vyama vya siasa Jaji Mstaafu Francis Mtungi kumuuliza kama ofisi yake imeona na kushuhudia UVCCM waliwakusanya watoto wa Sekondari kutoka mashuleni Jijini Dar es saalam na kuwapeleka katika shughuli za kisasa uwanja waTaifa
Simu ya Msajili wa vyama vya siasa imeita bila kupokelewa.