Mwanafunzi apeta Ubunge Kenya

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Aliyekuwa mgombea wa Ubunge Igembe Kusini nchini Kenya, John Mwirigi (24) ameshinda nafasi hiyo baada ya matokeo kutangazwa na Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).


Mwirigi ambaye anatajwa kuwa Mbunge mwenye umri mdogo kuwahi kutokea aliwashangaza wengi katika kampeni zake ambapo alikuwa akitumia baiskeli na bodaboda.


Mwirigi ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya elimu katika chuo cha Mount Kenya alikuwa mgombea binafsi hakuwahi kuwa na matangazo kwa kile kilichodaiwa kukosa pesa za kufanya kazi hiyo.
Katika matokeo hayo, Mwirigi alipata kura 18,867 huku mgombea wa Jubilee, Rufus Miriti akipata kura 15,411.
 
Kenya wametanguria mita 1000 kwa land cruiser sisi tupo nyuma tunawafukuzia kwa baiskeli

_ where ever you are remember me_
 
Kenya wametanguria mita 1000 kwa land cruiser sisi tupo nyuma tunawafukuzia kwa baiskeli

_ where ever you are remember me_
Hiyo hiyo baisikeli ndo kijana aliitumia kuwabwaga watu wa helikopta kwahivyo usife moyo budaboss! Hilo ndo funzo kutoka kwa huyo kijana. Hongera kwake mheshimiwa John Mwirigi! Kwa watu wa Meru na Igembe...Turishokia nkatho buru! Muritonyia kamwana vaai, Murunku amatharime bwinthe! Dah hii lugha ya kimeru ni stress!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…