Mwanafunzi apigwa risasi tumboni chuo kikuu cha dar es salaam usiku wa kuamkia leo

Mwanafunzi apigwa risasi tumboni chuo kikuu cha dar es salaam usiku wa kuamkia leo

pole yake lakini ni mjinga sana ,nani alimwambia hapa duniani kuna kitu kama hicho eti kuomba soft copy lol!
 
Poleni sana wanafunzi wa udsm kwa matatizo ya kuvamiwa.
 
mmmh usiseme hivyo ndg kama unayajua mazingira ya chuo na kuanda thesis si mchezo
 
nchi yetu inahitaji ulinzi wa hali ya juu pia vijana wawezeshwe waweze kujiajiri maana ndio hao hao wanavamia watu na kuwapora mali zao

Kuna kipindi wana udsm waishio mabibo hostel walikua wakiibiwa laptop, simu na vitu vingine vya thamani ikabidi waanze kuweka ulinzi shirikishi. Kilichotokea ni kukamatwa na kupigwa kwa wezi kadhaa hatimaye kuuawa na wizi ukapoa.

Sasa kwa tukio la hapo udsm leo naona wezi wamerudi tena kwa mtindo wa kutumia silaha za moto, amani imetoweka kabisa kwa wana udsm. Uongozi wa chuo usaidie kuimarisha ulinzi kwa wana udsm na mali zao.
 
tanzania kwa ujumla tuna amani ya mdomoni tuu lakini in reality hakuna amanii nchi imetawaliwa na rushwa na ujanjaujanja tuu inanuka damu za watu wasio na hatiia
 
Ushaona majambazi wana silaha,wanaondoka wanakuacha salama unaanza kuwadai soft copy!huyu msomi wa wp huyu.soft copy unapoteza maisha
 
mmmh usiseme hivyo ndg kama unayajua mazingira ya chuo na kuanda thesis si mchezo
pole yake ila maisha yake ni bora kuliko huko kuandaa thesis. nakumbuka mwaka 2006 nilikuwa nafanya kazi katika mradi mmoja dar kuna mzungu aliibiwa vifaa kwenye gari likatolewa tangazo ofisini kuwa mtu ukikutana nao hawa jamaa waache msibishane nao chochote wanachokitaka waache wachukue. ni vyombo vya dola tu vinatakiwa kubishana nao labda uwe umejihami uwataimu ila wakikutaimu achana nao na chochote wanachochukua unaweza kukipata tena ukiwa hai
 
tanzania kwa ujumla tuna amani ya mdomoni tuu lakini in reality hakuna amanii nchi imetawaliwa na rushwa na ujanjaujanja tuu inanuka damu za watu wasio na hatiia

Tumefika hapa tulipo kwa sababu ya kukosa viongozi wazalendo na wenye uchungu na wananchi wao. Mfano mdogo tu hebu angalia watu wanavyopigana vikumbo kuutafuta ubunge/urais/udiwani ndipo utaelewa nini namaanisha. Je, umeyaona/umeyasikia matokeo ya udiwani Arusha na kilichojiri? Je, umefuatilia kwa makini mgogoro wa mtwara na kilichotokea hatimaye jwtz kupiga kambi huko? Je, unazikumbuka ahadi za ajira kwa vijana zilizotolewa mwaka 2010 ukalinganisha na matukio purukushani kati ya wamachinga na polisi Mbeya, Mwanza na Arusha pengine na Dar?

Hapa ndipo tulipo ndugu yangu.
 
hahhahahahah kila kitu chademaaaa duuuh

Ninachoamini mimi ni kua hakuna uchadema wala uccm ktk mambo haya, ila yote yanatokea kwa sababu ya ubinafsi wa magenge ya watu wachache walioko kwenye mfumo wa utawala wa nchi.
Kumbuka kilichompata Ulimboka, Kibanda, na wengineo kisha utapata mwanga japo kidogo nini kilicho nyuma ya pazia.
Haya mambo ya uccm vs uchadema sijui uislam vs ukristo hayatokei kiuhalisia isipokua kuna genge/magenge nyuma ya pazia. Tuamke.
 
cku zote kama baba mwny nyumba ni mbwigga ndio matokeo yake ndio kule kusema akili ndogo inaongoza akli kubwa

Back
Top Bottom