Mwanafunzi apoteza maisha baada ya kupigwa kichwani na Mwalimu

Mwanafunzi apoteza maisha baada ya kupigwa kichwani na Mwalimu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Wazazi waliokuwa na hamaka walivamia shule ya msingi ya Gitithia eneo bunge la Lari wakitaka kukamatwa na kuzuiliwa kwa mwalimu aliyemtandika mwanafunzi ambaye baadaye aliaga dunia.

Mwanafunzi huyo aliyetambuliwa tu kama Wambui anasemekana alipigwa kichwani na mmoja wa walimu wakati alikuwa akinawa mikono yake nje ya darasa.

Mamake, Elizabeth Wanjiku, aliiambia NTV Wambui alilalamika kuhusu maumivu makali ya kichwa wakati aliporudi kutoka shule baadaye jioni hiyo. "Nilipomuuliza kwa nini alikuwa akihisi maumivu aliniambia alipigwa na mwalimu," alisema Wanjiku.

Familia ilisema matokeo ya upasuaji yalionyesha kuwa mwanao alipoteza maisha yake kutokana na majereha aliyopata baada ya kugongwa na kifaa butu kichwani. Wazazi waliokuwa na hasira walifanya maandamano nje ya shule hiyo wakidai haki kwa familia ya Wambui.

Iliwabidi maafisa wa polisi kuingilia kati na kuleta utulivu shuleni humo. Mwalimu mkuu wa shule hiyo Joseph Ndinguri alisema uchunguzi kuhusu suala hili umeanza na kuwataka wenyeji kuwa na subira.

"Sote tuna wasiwasi kwa sababu kifo cha mtoto ni jambo zito, nahisi uchungu pia lakini nataka kuwaomba wazazi wetu kuwa wavumilivu na subiri uchunguzi ukamilike ili tuweze kujua ni nini hasa kilitokea na hatua itakayofuata, " alisema Ndinguri.

Kisa hicho kilitokea wiki tatu baada ya mwanafunzi mwingine kufariki dunia katika Shule ya Msingi ya Lower Kihara katika eneo la Gashie, kaunti ya Kiambu.

Mtahiniwa huyo wa Darasa la Nane aliaga dunia baada ya kuanguka kutoka kwenye mlingoti wa bendera. Mwanafunzi huyo alikuwa amepanda kwenye mlingoti kuondoa kifaa kilichokuwa kimekwama juu baada ya kuagizwa na mwaliu wake.

Read more: Kiambu: Wazazi wazua fujo baada ya mwalimu kumpiga mwanafunzi hadi kufa
 
sijasoma habari yote ila bila shaka ni wale jilani waliopakana na somalia
 
Miss zomboko kakross boda,nkajua wewe habari za Tz pekee
 
Alikua na hasira kiasi gani huyo mwalimu? Mpaka unamdunda mtoto kichwani.
 
Back
Top Bottom