Mwanafunzi atuhumiwa kuua mwenzake chuoni

Mwanafunzi atuhumiwa kuua mwenzake chuoni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi Kange, jijini hapa anadaiwa kumuua mwanafunzi mwenzake kwa kumchoma kisu baada ya kumkuta kwenye chumba cha rafiki yake wa kike.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi, Blasius Chatanda, alithibitisha jana kwa njia ya simu kutokea kwa tukio hilo, na kueleza kuwa palitokea ugomvi baina ya wanafunzi wa kiume.

Ugomvi huo ulizuka juzi, baada ya kukutana kwenye chumba cha msichana huyo, huku kila mmoja akiona kuwa ana haki ya kummiliki msichana huyo.

Kwa mujibu wa Kamanda Chatanda, aliyefariki dunia katika tukio hilo ni Hussein Daud, ambaye anadaiwa alichomwa kisu na Waziri Ramadhan.

Alifafanua kuwa Daudi alikutwa ndani ya binti huyo.

“Huyu Hussein Daudi aliuawa kwa kuchomwa kisu na mtu anayedaiwa kuwa ni Waziri Ramadhan kwa sababu ya wivu wa mapenzi,” alisema na kuongeza:

"Walikutana kwenye chumba cha binti huyo, ndipo walipoanza kugombana wakidhani kuwa kila mmoja anayo haki ya kummiliki."

"Sasa katika ugomvi huo wakiwa chumbani kwa msichana huyo, Waziri Ramadhan alichukua kisu na kumchoma Daud na kusababisha kifo chake papo hapo."

Aidha, Kamanda Chatanda alisema tukio hilo haliwezi kufananishwa na tukio la fumanizi, na kwamba vijana hao wote wawili wamekatisha ndoto zao.

Kutokana na tukio hilo, Kamanda Chatanda aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo kwa kuwa hicho ndicho kilichowapeleka hapo.

Kamanda huyo alisema wanamshikilia binti huyo, huku mtuhumiwa akidaiwa kukimbia.

Chanzo: Nipashe

Pia soma > Imenishangaza: Dunia ya leo bado kuna wanaume wanapigana mpaka kuuana kisa mwanamke?
 
Mtu akimgusa huyu mrembo wangu huyu ni jambia wala siyo kisu!
876543.jpg
 
Madhara ya MMU haya, nimecheka kama mazuri lakini huo ni ujinga, yaani mtu unakatisha ndoto zako zote kwa kugombana kisa kabinti kamoja kadogo'dogo, alafu mwenyewe unakula pesa ya mama na baba,

someni kwanza hivyo vibinti vipo vinazaliwa kila siku, tena ukiwa na elimu yako na unajiweza utavipata vizuri zaidi na vingine vitakukimbiza.
 
Back
Top Bottom