Mwanafunzi darasa la pili apotea siku sita, mwili wake wakutwa pagalani

Mwanafunzi darasa la pili apotea siku sita, mwili wake wakutwa pagalani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwanafunzi aliyekuwa anasoma darasa la pili Shule ya Msingi Jitegemee Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoa wa Pwani nchini Tanzania (jina linahifadhiwa kwa sasa) amekutwa amekufa ndani ya nyumbani ambayo ujenzi wake bado haujakamilika.

Mwanafunzi huyo ambaye inadaiwa alipotea tangu Januari 14, 2020 na taarifa zake kutolewa na ndugu kwa Jeshi la Polisi mkoani Pwani inaelezwa mwili wake umekutwa na michubuko sehemu za siri tukio ambalo linaleta hofu kuwa huenda alifanyiwa vitendo vya ubakaji kabla ya kuuawa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amesema awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo aliondoka nyumbani kwao akiwa na shangazi yake, Agnes Peter kwenda gulioni maeneo ya Mwendapole kwa shughuli za biashara.

Wankyo amesema ilipofika saa 12 jioni, Shangazi yake huyo alimruhusu marehemu kwenda nyumbani akiwa peke yake kwaajili ya kufanya maandalizi ya shughuli za siku inayofuata.

Amesema shangazi yake alipofunga biashara zake na kurejea nyumbani hakumkuta marehemu na kuchukua hatua ya kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi juu ya tukio hilo pamoja na maeneo mengine ambapo jitihada za kumtafuta ziliendelea bila mafanikio hadi kukuta miwili wake ukiwa ndani ya jumba hilo juzi Januari 19,2020.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka watu waliohusika na kitengo hicho ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.

Polisi wamesema kwa sasa hawawezi kutaja jina la marehemu hadi hapo baadaye uchunguzi wao utakapokamilika.


Chanzo: Mwananchi
 
Daah! Jamani asa kweli katoto ka darasa la pili unakatendea unyama wa design hiyo? Kanaelewa nini asa...
 
RIP
Sijui ni wa kike au kiume!
Pumzika kwa amani katoto kazuri.
Washenzi watapatikana tu, damu yako haiwezi kwenda bure
 
Inauma sana sana.

Kama hatuwezi kunyonga, tungeingia mkataba na CHINA ili mtu akihukumiwa kifo akapewe adhabu huko. Nimewaza hivi kwa uchungu
 
Halafu eti adhabu ya kifo kwa kenge kama hao iondolewe! Shxnzie sana. Msimamo wa kizwazwa kabisa toka kwa wale ambao hawajawahi kuumizwa na wauaji.
 
Back
Top Bottom