Mwanafunzi wa chuo apigwa risasi na polisi, Mashuhuda waelezea tukio zima

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kiongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Meru nchini Kenya, Evans Njoroge ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi jana Februari 27,2018 katika maanadamano chuoni hapo wakishinikiza chuo hicho kupunguza ada yao kwa kiasi cha shilingi 8,500 za Kenya ambazo ni sawa na Tsh 188,566 na kuboreshewa miundombinu chuoni hapo.

Mashuhuda wa tukio hilo waliohojiwa na kituo cha runinga cha NTV wamesema kuwa wanafunzi wa chuo hicho baada ya vurugu walikimbia nje ya chuo na kwenda kujificha mashambani baada ya kuona gari la polisi.

Shuhuda mmoja ambaye mwanafunzi huyo ameuawa kwenye shamba lake la viazi vitamu, amesema kuwa maaskari baada ya kuwakosa chuoni walikuja uraiani walipomuuliza kama amewaona wanafunzi hao alikataa kuwajibu, lakini baadaye mtoto wake aliwaelekeza polisi wanafunzi hao walipojificha.

Baada ya dakika mbili mama huyo ambaye jina lake halijatajwa kwa sababu za kiusalama alisema alisikia mlio wa bunduki na alipotoka alimkuta askari anabadilisha mavazi yake na kubakia na nguo za kiraia.

Niliona wanafunzi wakikimbia nje ya geti la nyumba yangu wengine wakielekea mashambani, muda mfupi baadae nikaona polisi wakiingia getini kwangu wakiniulizia walikojificha sikuwajibu! hadi mtoto wangu alipowaambia, baadaye baada ya kumuona mwanafunzi huyo amejificha kwenye mti alimpiga risasi wakati alipotaka kumkimbia na akabadilisha nguo zake na kurudi kwenye gari,“amesema shuhuda kwenye mahojiano yake na Kituo cha NTV Kenya.

Kwa upande wa mashuhuda wengine wamesema kuwa polisi huyo aliyemuua mwanafunzi anafahamika ni Afisa wa jeshi la polisi la kituo cha Nchiru.

Taarifa kutoka kituo kingine kikubwa cha polisi cha Tigania, kupitia kwa msemaji mkuu wa kituo hicho, Kamanda Adamson Furaha amesema kuwa alisikia kuna maandamano na alituma polisi wa kuzuia maandano hayo.

Kwa upande wa uongozi chuoni hapo umesema kuwa umepata taarifa hizo na mwili wa mwanafunzi umepelekwa Hospitali kwa ajili ya majibu ya kitabibu. Tazama video aliyorekodiwa kabla kuuawa muda mfupi baadaye.

Hata hivyo baada ya tukio hilo wanafunzi waliendelea kushinikiza makamu wa Rais wa chuo hicho, Japheth Magambo kujiuzulu nafasi yake kwani ndiye anayeharibu chuo hicho. Baadhi ya Wakenya wakiwemo viongozi na wanaharakati wamelaani vikali tukio hilo la askari kujichukulia sheria mkononi, wengi wakisema kuwa ni tukio la kinyama.

Tayari jeshi la polisi nchini Kenya linafanya uchunguzi juu ya tukio hilo, na Chuo hicho kilichotakiwa kufunguliwa leo Februari 28, 2018 kupitia mtandao wake kimatangaza kuahirisha hadi Machi 6, 2018.

Bongo 5
 
Unyama wa polisi wa Kenya hauna mfano hapa Afrika na dunia nzima, watu wameshakimbia na kujificha, bado mnawasaka na kuwapiga risasi kinyama kabisa, Kenya is really a failed state.
 
Kwa Kenya hii wala siyo habari labda wanafunzi ndiyo wangeua polisi.

Jungle justice as usual.

Only the strong will get survival.

Nawapa pole SANA wazazi, maana mtoto akifikia kiwango hicho unahesabia umetua mzigo.
 
Ingekuwa ni Tz mashuhuda wangekuwa walishafunga safari ya kuhamia kule Kinshasa, DRC, tena zamani sana.
 
Ingekuwa ni Tz mashuhuda wangekuwa walishafunga safari ya kuhamia kule Kinshasa, DRC, tena zamani sana.
Badala ya kuungana na kulaani polisi wenu wenye sifa ya kuwapiga risasi kila siku, unazungumzia upuuzi, hujui kwamba Kenya police killings is top in Africa, and among top 5 in the World?
 
Nakuhakikishia kwa tukio hili, wakenya wataandamana kama wapalestina kudai haki ya mwanachuo huyo, Huku kwetu watu wangekimbilia kwenye social mediaz kupiga kelele tena kwa kuombwa id zao zisiwekwe wazi......INATIA HASIRA SANA HII
 
Leo ni siku ya pili hata kulizungumzia hawalizungumzii, lini wataadamana, au wanasubiri sherehe zao za sikukuu ya jamhuri ndiyo waunganishe maandamano yawe makubwa?. Chris Msando na Jacob Juma walipouliwa, mbona hawakuandamana, watu 60 waliouliwa katika vipindi vya uchaguzi, mbona wanazika wafu wao kimya kimya hawaandamani?. Nafuu Tanzania alipokufa Akwilina watu walipaza sauti na serikali japo iliomba radhi, Kenya hata hawazungumzi lolote, kwanza wajaluo wanafurahi kwasababu huyo mwanafunzi ni mkikuyu, kamwe usilinganishe Kenya na Tanzania katika eneo hilo.
 
Nakuhakikishia kwa tukio hili, wakenya wataandamana kama wapalestina kudai haki ya mwanachuo huyo, Huku kwetu watu wangekimbilia kwenye social mediaz kupiga kelele tena kwa kuombwa id zao zisiwekwe wazi......INATIA HASIRA SANA HII
Unazungumzia Kenya gani, ile ya da'Mange?
 
Nakuhakikishia kwa tukio hili, wakenya wataandamana kama wapalestina kudai haki ya mwanachuo huyo, Huku kwetu watu wangekimbilia kwenye social mediaz kupiga kelele tena kwa kuombwa id zao zisiwekwe wazi......INATIA HASIRA SANA HII
Sahau, tuone kama wataandamana.
 
Ingekuwa ni Tz mashuhuda wangekuwa walishafunga safari ya kuhamia kule Kinshasa, DRC, tena zamani sana.
nilidhani kwetu, duh
Kwa Kenya hii wala siyo habari labda wanafunzi ndiyo wangeua polisi.

Jungle justice as usual.
Unyama wa polisi wa Kenya hauna mfano hapa Afrika na dunia nzima, watu wameshakimbia na kujificha, bado mnawasaka na kuwapiga risasi kinyama kabisa, Kenya is really a failed state.
wepesi kusahau huh?

How safe is Tanzania? Tanzanian girl student brutally shot dead in political chaos - eTurboNews (eTN)

Tanzania's opposition accuse police of killing student
 
Huo ndiyo ujinga wenu ulipolala, hamkuona jinsi watanzania na serikali walivyowajibika baada ya hilo unfortunate event?, kwanza haikuwa intended kumuua kwa hiyo ni kosa kusema brutally murdered labda kama kiingereza hukijui vizuri, it was accidentally murdered, huyu mwanafunzi wa Meru ndiyo brutally murdered.

Tuachozungumza hapa ni reactions baada ya tukio, wakati Tanzania nzima shughuli zilikaribia kusimama kutokana na hicho kifo cha bahati mbaya, huko kwenu hamjali na hakuna mtu anayeshughulika kwa kifo cha makusudi kabisa, wakati huko DRC wamemfunga kifungo cha maisha askari aliyempiga risasi na kumuua muandamanaji, huko kwenu hata uchunguzi hakuna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…