Mwanafunzi wa Chuo na baba yake

Red Scorpion

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,736
Reaction score
4,252
Dogo mmoja alifanikiwa kuingia chuo kimojawapo nchini kwa mbwembwe sana. Katikati ya semista, dogo akaishiwa hela na akaamua kumwandikia baba yake barua.

"Kwako baba,

Ni matumaini yangu hujambo. Huku chuoni mambo ni mazuri sana. Kuna maajabu hapa maprofesa hapa wamegundua njia ya kufundisha mbwa kuongea. Mlete Bobi na shilingi laki 5, baada ya muda atakuwa anaweza kuongea.

Ni mimi mwana'ko Dogo."

Mzee wa watu haraka akatuma mkwanja na mbwa wake chuoni. Haikuchukua muda mkwanja ukaisha. Dogo akamtumia baba yake barua nyingine kuwa walimu wameboresha programu kwani sasa wanaweza kumfundisha mbwa kusoma.

Mzee wa watu akaongeze kimilioni bila hiyana. Mzee huyu aliyekuwa tayari anajisifu kijiji kizima akauza ng'ombe akatuma mkwanja. Likizo ikafika Dogo akabaki anawaza anaenda kumwambia nini baba yake.

Alipofika tu baba yake akamuulizia Bobi wake. Dogo akamuita baba yake pembeni.

#Dogo: Baba hili nitakalokwambia sitaki mama asikie.
[URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=Baba%3A]#Baba: Vipi[/URL] tena?
#Dogo: Jumapili iliyopita tumeamka vizuri na Bobi, yeye kama kawaida yake akaenda kuchukua gazeti la Mzalendo na kukaa kwenye kiti na kuanza kusoma, ghafla wakati anasoma akaniita
akanambia hivi,

"baba yako bado anaendelea na kale kachangudoa ka pale mtaa wa pili?"

Nilishtuka!

#Baba: (Akaingilia kati) Ungemwua hapo hapo mbwa mshenzi huyu anataka kuniharibia mambo yangu!
#Dogo: Baba na mimi lilinijia wazo hilo hilo, sikumchelewesha nikamtwanga nyundo ya kichwa!

Baba: Safi sana, safi sana, wewe jembe langu!
 
Ha ha ha ha ha ha ha umetisha mkuu
 
Hahaha haha you made my day
 

Nooooooomaaaaa
 
Aaaaah ilo ndo tatzo la kuwapga elimu wazaz wetu
 
Teh Teh Teh Teh chuo gani icho namim nimpeleke mbwa wangu?
 
Chuo gani icho namim nimpeleke mbwa wangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…